Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Maumivu ya tumbo, upande wa kulia chini ya mbavu


Sio kila dalili za maumivu ya tumbo upande wa kulia yanasababishwa na changamoto ya homa ya ini.

Maumivu ya tumbo upande wa kulia chini ya mbavu yanaweza kusababishwa na hali mbalimbali, kwa sababu eneo hilo lina viungo muhimu kama ini, nyongo, sehemu ya utumbo, figo ya kulia, na pia misuli ya eneo hilo.

 

Baadhi ya Sababu kuu zinazoweza kusababisha maumivu hayo:

 

1. Magonjwa ya ini – mfano hepatitis (homa ya ini), fatty liver, au cirrhosis.

 

2. Mawe kwenye nyongo (Gallstones) – huleta maumivu makali ghafla baada ya kula vyakula vyenye mafuta.

 

3. Cholecystitis – uvimbe wa kibofu cha nyongo.

 

4. Maambukizi ya virus au minyoo - kama vile viru vya homa ya ini na minyoo ya kichocho au majipu (liver abscess).

 

5. Ugonjwa wa kongosho (pancreatitis) – hasa ukihusisha sehemu ya kichwa cha kongosho kilicho karibu na upande wa kulia.

 

6. Magonjwa ya utumbo – mfano appendicitis (wakati kidole tumbo kimepanda juu), au colitis.

 

7. Figo ya kulia – mawe ya figo, maambukizi (pyelonephritis).

 

8. Maumivu ya misuli au mbavu – majeraha au msukosuko wa misuli ya mbavu.

 

9. Ujauzito - kama vile ujauzito wa mimba changa au matatizo ya mimba (kwa wanawake).

 

10. Saratani – ya ini, nyongo au kongosho (kwa hali nadra zaidi).

 

Baadhi ya Dalili za kuzingatia (zinaweza kusaidia kutofautisha chanzo):

 

✔️ Kichefuchefu/kutapika → mara nyingi huashiria tatizo la nyongo au ini.

 

✔️ Kuhisi uzito au uvimbe tumboni → linaweza kuashiria ini limepanuka.

 

✔️ Kikohozi au maumivu yakiongezeka ukipumua → huweza kuwa tatizo la mapafu juu ya ini.

 

✔️ Homa na baridi → maambukizi (kibofu cha nyongo, ini au figo).

 

✔️ Mkojo wa giza/macho ya manjano → matatizo ya ini au nyongo.

 

✔️ Maumivu baada ya kula vyakula vya mafuta → mara nyingi mawe kwenye nyongo.

 

✔️ Maumivu makali yanayoelekea mgongoni au bega → matatizo ya nyongo au kongosho.

 

 

Baadhi ya vipimo vinavyosaidia kutambua chanzo cha tatizo:

 

✔️ Kipimo cha Ultrasound ya tumbo (kuchunguza ini, nyongo, figo).

 

✔️ Vipimo vya damu vya ini (LFTs) – ALT, AST, ALP, bilirubin.

 

✔️ Vipimo vya figo (RFTs) – Urea, creatinine, electrolytes.

 

✔️ Complete blood count (CBC) – kutambua maambukizi.

 

✔️ CT scan/MRI – kama tatizo halijulikani vizuri.

 

✔️ Urinalysis – kuangalia mawe au maambukizi ya figo.

 

❗Kwa kuwa maumivu upande huo yanaweza kuwa dalili ya kitu cha dharura (mfano mawe kwenye nyongo, homa ya ini, au mawe kwenye figo), ni muhimu kumwona daktari mapema hasa ikiwa yanaambatana na homa, kutapika, ngozi/macho kuwa manjano, au maumivu makali yasiyopungua.

 

kwa huduma za matibabu na ushauri, usisite kuwasiliana nasi kwakupiga simu au kutuna ujumbe mfupi wa maandishi kupitia whatsap +255628361104 +255746484873

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!