Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Ugonjwa wa U.T.I, visababishi na dalili za awali na athari zake


Ugonjwa wa U.T.I usipo tibiwa husababisha madhara makubwa ya kiafya hasa kwa wanaume


FAHAMU KWAKINA UGONJWA WA U.T.I - U.T.I NI NINI?

 

  • Ugonjwa wa UTI ni maambukizi yanayotokea katika sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo (maambukizi katika njia ya mkojo). Mfumo huu unajumuisha figo, mirija ya mkojo (ureters), kibofu na urethra.

     

  • Maambukizi mengi hutokea katika sehemu za chini za mfumo wa mkojo — yaani kibofu na urethra.

     

  • Wanawake wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata UTI kuliko wanaume. Ikiwa maambukizi yatabaki kwenye kibofu tu, huweza kuwa na maumivu na usumbufu. Hata hivyo, matatizo makubwa ya kiafya yanaweza kutokea ikiwa maambukizi yataenea hadi kwenye figo.

     

  • Watoa huduma za afya mara nyingi hutibu UTI kwa kutumia antibiotiki. Pia, unaweza kuchukua hatua mbalimbali ili kupunguza hatari ya kupata UTI.

 

BAADHI YA DALILI ZA UGONJWA WA U.T.I

 

UTI haziwezi kuonesha dalili za moja kwa moja kila wakati. Lakini zikijitokeza, zinaweza kujumuisha dalili hiizi zifuatazo:

 

  • Hisia ya kuhitaji kukojoa mara kwa mara zisizokwisha

     

  • Maumivu wakati wa kukojoa (Kama mkojo unaunguza)

     

  • Kukojoa mara kwa mara huku ukitoa mkojo kidogo sana
     

  • Mkojo unaoonekana na ukungu (Mawingu mawingu)

     

  • Mkojo wenye rangi nyekundu, waridi mkali au kama soda ya coca cola —Hii ni  ishara ya damu kwenye mkojo Kuontesha kuwa huenda maambukizi yamefika kwenye figo.

     

  • Kupata Mkojo wenye rangi na harufu kali

 

Kwa watu wazima waliozeeka, UTI huweza kufichika au kuchanganywa na hali nyingine za kiafya.

 

UTI sugu ni hali ambapo mtu hupata maambukizi ya njia ya mkojo mara kwa mara, kwa mfano:

 

  • Mara mbili au zaidi ndani ya miezi 6

     

  • Au mara tatu au zaidi ndani ya mwaka mmoja

 

BAADHI YA VISABABISHI VYA UGONJWA WA U.T.I IKIWA IMEFIKA KWENYE KIBOFU:


  • Aina hii ya UTI mara nyingi husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli),wanaopatikana kwa kawaida katika mfumo wan jia ya haja kubwa (Mkundu). Lakini mara nyingine, bakteria wengine huweza kuwa chanzo.

 

  • Kufanya ngono pia kunaweza kusababisha maambukizi kwenye kibofu, lakini si lazima uwe unajamiiana ili kupata maambukizi. Wanawake wote wapo katika hatari ya kupata UTI kutokana na muundo wa miili yao.

 

  • Urethra ya mwanamke ipo karibu na mkundu, na pia karibu na kibofu (ni fupi sana). Hali hii hurahisisha bakteria kutoka kwenye mkundu kuingia kwenye urethra na kufika hadi kwenye kibofu.

     

  • Maambukizi Haya hutokea pale ambapo bakteria kutoka kwenye mfumo wa chakula na husambaa hadi kwenye urethra (mrija wa mkojo). Pia, magonjwa ya zinaa kama vile herpes, kisonono, chlamydia na mycoplasma yanaweza kusababisha maambukizi ya urethra, hasa kwa sababu urethra ya wanawake ipo karibu na uke.

 

  • Matatizo ya kuzaliwa ya njia ya mkojo: Watoto wanaozaliwa na matatizo kwenye mfumo wa mkojo wanaweza kuwa na matatizo ya kutoa mkojo, hivyo mkojo hurudi nyuma na kusababisha UTI.

     

  • Vizuizi kwenye njia ya mkojo: Mfano kama una Mawe kwenye figo au kibofu kilichojaa kutokana na mkojo kukwama kwa mgonjwa wa tezi dume huweza kuongeza hatari ya uti.

     

  • Upungufu wa kinga mwilini: Magonjwa kama kisukari hupunguza kinga ya mwili na kuongeza uwezekano wa kupata UTI.

     

  • Matumizi yatokanayo na katheta: Watu wasioweza kukojoa wenyewe hutumia mirija ya kutoa mkojo (katheta), ambayo huongeza hatari ya UTI.

 

  • Upasuaji wa njia ya mkojo au vipimo vya ndani vya mfumo wa mkojo vinaweza pia kuongeza uwezekano wa maambukizi.

 

Hatua hizi zinaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata UTI:

 

  • Kunywa maji ya kutosha, hasa maji safi. Husaidia kufuta mkojo mara kwa mara na kuondoa bakteria.

     

  • Jaribu juisi ya cranberry. Tafiti kuhusu faida zake bado hazijathibitisha moja kwa moja, lakini ina matokeo makubwa katika kusafishanjia ya mkojo.

 

  • Jisafishe kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kujisaidia haja kubwa ili kuzuia kueneza bakteria kutoka mkunduni hadi ukeni au kwenye urethra.

     

  • Kojoa mara baada ya tendo la ndoa. Pia kunywa glasi ya maji ili kusaidia kuosha bakteria, watoke nje kwa urahisi.

     

  • Epuka kutumia bidhaa zinazokera sehemu za siri, vitu kama dawa za kunyunyiza manukato, dawa za kusafisha uke, Pamoja na poda.

     

  • Badilisha njia ya uzazi wa mpango. Diaphragms, kondomu zisizo na vilainishi, au zenye dawa ya kuua mbegu huweza kuchangia kukua kwa bakteria wengi zaidi ambao huleta shida ya uti.

 

BAADHI YA MADHARA YA UGONJWA WA U.T.I ISIPO TIBIWA MAPEMA 

 

  • Uharibifu wa kudumu wa figo

     

  • Figo kuferi hadi kufikia hatari ya matibabu ya Kuhitaji dialysis

     

  • Uzazi wa watoto wenye uzito mdogo au kuzaa kabla ya wakati

     

  • Prostatitis kwa wanaume

     

  • Sepsis (sumu katika damu)

     

  • Matatizo ya moyo

     

  • Shinikizo la damu la juu


KARIBU KATIKA MATIBABU

 

  • Ushauri wa madaktari bingwa ndani ya dakika chache kupitia clinic ya AFYA YANGU

     

  • Mpango wa matibabu salama unaofaa hali yako

     

  • Ufuatiliaji wa karibu na madaktari wakati wa tiba

     

  • Ushauri wa kuzuia UTI kurudi tena

 



DAWA ZA MATIBABU YA U.T.I


  • Probiotics (soma makala kuhusu probiotics)

     

  • Maji ya mgogoro

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!