Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Faida za juice ya miwa, hutumika kama kikata kiu na kisafisha Damu


Juice ya miwa ni kinywaji kinachotengenezwa kutokana na maji yanayokamuliwa kutoka kwenye miwa.

๐—ง๐—จ๐— ๐—œ๐—” ๐—๐—จ๐—œ๐—–๐—˜ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—œ๐—ช๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฆ๐—”๐—™๐—œ๐—ฆ๐—›๐—” ๐——๐—”๐— ๐—จ ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ž๐—จ๐—ข๐—ก๐——๐—ข๐—” ๐—ฆ๐—จ๐— ๐—จ ๐—ก๐—” ๐—ž๐—จ๐—ข๐—ก๐—š๐—˜๐—ญ๐—” ๐—ก๐—œ๐—ฆ๐—›๐—”๐—ง๐—œ ๐—ž๐—ช๐—˜๐—ก๐—ฌ๐—˜ ๐—ฆ๐—˜๐—Ÿ๐—œ ๐—ญ๐—”๐—ž๐—ข:


Juice ya ni tamu kiasili na mara nyingi hunywewa freshi bila kuongeza viambato vingine, ingawa wengine huongeza limao, tangawizi, au minti kwa ladha zaidi.

 



Ni maarufu sana katika nchi za tropiki, hasa Afrika, Asia, na Amerika ya Kusini, kwa sababu ya ladha yake tamu na uwezo wake wa kupooza mwili hasa wakati wa joto.

 

Pia juice ya miwa ina faida kadhaa za kiafya kama vile kutoa nishati ya haraka, kusaidia mmengโ€™enyo wa chakula, na kuwa na virutubisho kama madini na antioxidants.


Kwa wagonjwa kama vile Mgonjwa Presha, mapafu, figo na mgonjwa wa homa ya ini (hepatitis) hushauriwa kutumia juice ya miwa kwa sababu mbali mbali zifuatazo:

 

๐—›๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐˜€๐—ต๐˜‚๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ฆ๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ถ๐—ธ๐—ถ๐˜‡๐—ผ ๐—น๐—ฎ ๐——๐—ฎ๐—บ๐˜‚:

Juisi ya miwa ina potasiamu, ambayo husaidia kupunguza msongo wa mishipa ya damu (vasodilation), hivyo kusaidia kupunguza shinikizo la damu.

 

๐—œ๐—ป๐—ฎ๐—ฏ๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐— ๐˜‡๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚๐—ธ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐——๐—ฎ๐—บ๐˜‚:

Virutubisho vilivyomo kwenye juisi ya miwa vinaweza kusaidia kuimarisha afya ya moyo na mishipa ya damu kwa kuboresha mzunguko wa damu.

 

๐—›๐—ฎ๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐— ๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐˜๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—–๐—ต๐—ผ๐—น๐—ฒ๐˜€๐˜๐—ฒ๐—ฟ๐—ผ๐—น:

Juisi ya miwa ni chanzo asili cha nishati bila mafuta mabaya au cholesterol, hivyo ni salama kwa afya ya moyo na tishu kwa ujumla.

 



๐—œ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐—ธ๐—ถ๐—ธ๐˜‚๐—ฏ๐˜„๐—ฎ ๐˜€๐—ฎ๐—ป๐—ฎ ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ ๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ถ๐—ผ๐˜…๐—ถ๐—ฑ๐—ฎ๐—ป๐˜๐˜€ (๐—ฉ๐—ถ๐—ผ๐—ป๐—ฑ๐—ผ๐—ฎ ๐˜€๐˜‚๐—บ๐˜‚):

Juisi ya miwa ina antioxidants, ambazo hupambana na madhara ya radicali huru zinazoweza kuharibu mishipa ya damu na kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo, ini, figo, utumbo, kongosho,  nyongo na ubongo.

 

๐—›๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐—ฑ๐—ต๐—ถ๐—ฏ๐—ถ๐˜๐—ถ ๐—ฉ๐—ถ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐˜ƒ๐˜†๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—ธ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—ฑ๐—ฎ๐—บ๐˜‚:

Ingawa ina sukari ya asili, juisi ya miwa ina index ya chini ya glycemic, ambayo inamaanisha haipelekei ongezeko la ghafla la sukari kwenye damu, jambo muhimu kwa wagonjwa wa presha, ini na kisukari.

 

๐—›๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐—น๐—ถ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ถ๐—บ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ฎ๐—ณ๐˜†๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—œ๐—ป๐—ถ:

Juice ya miwa ina virutubisho kama antioxidants, vitamini na madini yanayosaidia kupunguza mzigo wa sumu kwenye ini na kulisaidia kujijenga upya ini.

 

๐—๐˜‚๐—ถ๐—ฐ๐—ฒ ๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐˜„๐—ฎ ๐—ต๐˜‚๐—ถ๐—บ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ก๐—ด๐˜‚๐˜ƒ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ ๐˜€๐—ฒ๐—น๐—ถ ๐—ฝ๐—ฎ๐—บ๐—ผ๐—ท๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐— ๐˜„๐—ถ๐—น๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐˜‚๐—ท๐˜‚๐—บ๐—น๐—ฎ:

Wagonjwa wa homa ya ini mara nyingi hukosa nguvu kutokana na ini kushindwa kufanya kazi vizuri.

Juice ya miwa ni chanzo kizuri cha nishati ya haraka mwilini kutokana na sukari asilia iliyo ndani yake.


 


๐—๐˜‚๐—ถ๐—ฐ๐—ฒ ๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐—ถ๐˜„๐—ฎ ๐—ป๐—ถ ๐—บ๐˜‚๐—ต๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ณ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—œ๐—ป๐—ถ:

Juice hii husaidia kuondoa sumu mwilini, hivyo kupunguza mzigo wa kazi kwa ini na kusaidia kupona haraka.

 

๐—›๐˜‚๐—ฏ๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—บ๐—ณ๐˜‚๐—บ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐—บ๐—ฒ๐—ป๐—ดโ€™๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—–๐—ต๐—ฎ๐—ธ๐˜‚๐—น๐—ฎ

Wagonjwa wa homa ya ini mara nyingi hukabiliwa na matatizo ya mmengโ€™enyo wa chakula. Juice ya miwa ina alkali inayosaidia kuweka mazingira bora ya usagaji wa chakula tumboni.

 

๐—›๐˜‚๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—จ๐˜‡๐—ฎ๐—น๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐˜„๐—ฎ ๐——๐—ฎ๐—บ๐˜‚ โ€“

Wagonjwa wa homa ya ini mara nyingi hupoteza hamu ya kula, jambo linaloweza kusababisha upungufu wa damu.

Juice ya miwa ina madini ya chuma (iron) na folic acid ambayo husaidia uzalishaji wa seli nyekundu za damu.

 

๐—›๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐—ฝ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ป๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐— ๐—ฎ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐˜‚๐—ธ๐—ถ๐˜‡๐—ถ โ€“

Miwa ina virutubisho kama flavonoids na phenolic compounds vinavyosaidia mwili kupambana na virusi na bakteria, hivyo kuimarisha kinga ya mwili.

Hata hivyo, wagonjwa wa homa ya ini wanapaswa kuweka kipaumbele matumizi sahihi ya vitu vya asili kama vile juice ya miwa, maji ya madafu, tangawizi, limau, matunda na mboga za majani.


 



๐—ž๐—จ๐— ๐—•๐—จ๐—ž๐—”:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


๐—ž๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ๐—ฏ๐˜‚ ๐˜๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ต๐˜‚๐—ฑ๐˜‚๐—บ๐—ถ๐—ฒ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ๐—บ๐—ผ๐˜๐—ผ ๐˜‡๐—ฎ ๐—ฎ๐—ณ๐˜†๐—ฎ ๐˜๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐˜๐—ผ๐—ฎ ๐—ต๐˜‚๐—ฑ๐˜‚๐—บ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—ฉ๐—œ๐—ฃ๐—œ๐— ๐—ข, ๐—จ๐—ฆ๐—›๐—”๐—จ๐—ฅ๐—œ ๐—ก๐—” ๐— ๐—”๐—ง๐—œ๐—•๐—”๐—•๐—จ.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!