Tafuta

Appointiment


*

Ratiba kamili, ya lishe bora siku nzima - Ni nzuri kwa wagonjwa wa homa ya ini, Figo, Kisukari na Shinikizo la damu (Presha)


Lishe bora na salama, ni sehemu ya matibabu katika kuongeza ufanisi wa mwili kutoa sumu mwilini, kudhibiti viwango vya chumvi, sukari, mafuta, protini na kinga ya mwili, Mazingatio ya lishe salama na matibabu ni hatua bora katika kuujenga mwili dhidi ya kujitibu majerehaa na kuondoa maambukuzi ya muda mlefu. Kama vile bakteria, virus na fangasi


𝗥𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔 𝗕𝗢𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗟𝗜𝗦𝗛𝗘 𝗬𝗔 𝗦𝗜𝗞𝗨 𝗡𝗭𝗜𝗠𝗔 - 𝗞𝗪𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗚𝗔𝗠𝗢𝗧𝗢 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗙𝗨𝗠𝗢 𝗪𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔:


Hii hapa ni ratiba ya mlo wa siku nzima kwa mtu mwenye changamoto ya afya ya ini na mfumo wa chakula.

Inalenga kukupatia virutubisho vya kutosha, nguvu na kusaidia ini kufanya kazi vizuri bila shida yoyote mbali na apo na kusaidia katika kupona haraka ikiwa pia upo katika matibabu bila kuliweka ini kwenye mzigo mkubwa wa madhara kama vile kuvimba.


🕗 𝗔𝘀𝘂𝗯𝘂𝗵𝗶 (𝟳:𝟬𝟬 - 𝟴:𝟬𝟬 𝗔𝗠): 𝗞𝗶𝗮𝗺𝘀𝗵𝗮 𝗸𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮

Inapo fika asubui pata kifungua kinywa


𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮:

 

  • Uji wa mtama au ulezi (usiwe na sukari nyingi, unaweza tumia asali kiasi)

     

  • Parachichi au kipande cha papai safi

     

  • Yai moja lililochemshwa

     

  • Kikombe cha maziwa yaliyochemshwa (yasiyo na mafuta mengi)


𝗞𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶:

 

  • Glasi moja ya maji ya uvuguvugu


🕙 𝗦𝗮𝗮 𝟰 𝗮𝘀𝘂𝗯𝘂𝗵𝗶 (𝟭𝟬:𝟬𝟬 𝗔𝗠): 𝗞𝗶𝘁𝗮𝗳𝘂𝗻𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗲𝗽𝗲𝘀𝗶

 

  • Ifikapo asubui mida ya saa nne unaweza ukapata kitafunwa chepesi.


𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮:

 

  • Tunda moja (kwa mfano: apple, embe, au tikitimaji)

     

  • Au karanga mbichi zilizochemshwa (kiasi kidogo)


𝗞𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶:

 

  • Maji safi ya kunywa au juisi ya matunda ya asili isiyo na sukari (mfano: juice ya papai, embe na pesheni, tango, au tikitimaji)


🕛 𝗠𝗰𝗵𝗮𝗻𝗮 (𝟭:𝟬𝟬 - 𝟮:𝟬𝟬 𝗣𝗠): 𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝗸𝗶𝗸𝘂𝘂 𝗰𝗵𝗮 𝗺𝗰𝗵𝗮𝗻𝗮

 

  • Muda wa mchana kuanzia saa saba hadi saa nane ni vizuri kula kiasi kidogo cha chakula.


𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮:

 

  • Wali au ugali wa dona / uwele / mtama

     

  • Mboga za majani zilizochemshwa vizuri (mfano: mchicha, kisamvu, spinach, tembele au sukuma wiki)

     

  • Samaki au kuku wa kienyeji aliyechemshwa au kuokwa bila mafuta maana yake asie kaangwa

     

  • Ndizi au viazi vilivyochemshwa vinaweza kuchukua nafasi ya wanga pia


𝗞𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶:

 

  • Maji ya kunywa au juisi ya asili isiyo na sukari


🕒 𝗦𝗮𝗮 𝟵 𝗮𝗹𝗮𝘀𝗶𝗿𝗶 (𝟯:𝟬𝟬 - 𝟰:𝟬𝟬 𝗣𝗠): 𝗞𝗶𝘁𝗮𝗳𝘂𝗻𝘄𝗮 𝗸𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲

 

  • Muda wa saa tisa ya jioni hadi saa kumi kamili.


𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮:

 

  • Kipande kidogo cha parachichi au mtindi usio na sukari

     

  • Mkate wa ngano uliochomwa bila mafuta hizi ni nafaka zisizo na sukari ndani yake ivyo salama kabisa.


𝗞𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶:

 

  • Maji au juisi ya embe/papai (kiasi)


🕖 𝗨𝘀𝗶𝗸𝘂 (𝟳:𝟬𝟬 - 𝟴:𝟬𝟬 𝗣𝗠): 𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝗰𝗵𝗮 𝘂𝘀𝗶𝗸𝘂

 

  • Ifikapo usiku kuanzia saa moja hadi saa mbili ya usiku


𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮:

 

  • Supu ya mboga za majani, samaki wa kuchemsha au supu ya kuku wa kienyeji.

     

  • Viazi vitamu, magimbi, maboga, mihogo ya kuchemsha au ndizi zilizochemshwa

     

  • Kachumbari au matunda kama tikitimaji kwa kumalizia


𝗞𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶:

 

▪️Glasi moja ya maji


🛏️ 𝗞𝗮𝗯𝗹𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗹𝗮𝗹𝗮 (𝘀𝗮𝗮 𝟭𝟬 - 𝟭𝟭 𝗷𝗶𝗼𝗻𝗶):

 

  • Kabla ya kulala na kupitiwa na usingizi yani ule muda unahitaji kupanda kitandani jitahidi upate mlo huu mwepesi ndopo ulale.


𝗞𝗶𝗻𝘆𝘄𝗮𝗷𝗶:

 

  • Glasi ya maji ya uvuguvugu au kikombe cha chai ya tangawizi/limao (bila maziwa)

 

⚠️ 𝗩𝗜𝗗𝗢𝗞𝗘𝗭𝗢 𝗠𝗨𝗛𝗜𝗠𝗨:

 

  • Epuka vyakula vya kukaanga na vyenye mafuta mengi.

     

  • Punguza chumvi na sukari nyingi.

     

  • Epuka soda, pombe, kahawa, na vyakula vya kusindika.

     

  • Kula mara kwa mara kwa kiasi kidogo ili kusaidia ini kufanya kazi vizuri.

     

  • Hakikisha unapata maji ya kutosha siku nzima (angalau glasi 6–8).


🥦 Lishe bora huendana na matibabu bora, kwapamoja hutoa suluhisho lililo bora na lakudumu katika kupona.

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.

 

𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!