Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Ugonjwa wa vidonda vya tumbo, sababu, dalili, madhara na matibabu


Ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni hali ambapo hutokea majeraha au vidonda kwenye ukuta wa ndani wa tumbo (stomach) au sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenum). Hali hii hujulikana kitaalamu kama:

Gastric ulcer - Kidonda kilichopo kwenye tumbo




Duodenal ulcer - kidonda kilichopo kwenye utumbo mdogo sehemu ya juu karibu na ini.


NOTE: Ukihitaji matibabu salama ya vidonda vya tumbo na lishe bora kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo, karibu kwa huduma tunaweza kukusaidia zaidi.


VISABABISHI VYA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO



1. Maambukizi ya bakteria Helicobacter pylori (H. pylori)  ndiyo sababu kubwa.


2. Magonjwa ya ini yasiyo tibiwa kwa muda mlefu na magonjwa ya mfumo wa chakula


3. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kupunguza maumivu kama aspirin, ibuprofen, na diclofenac.


4. Msongo wa mawazo (stress)  hasa ukiambatana na ulaji duni.


5. Unywaji wa pombe kupita kiasi huongeza asidi tumboni.


6. Uvutaji sigara, huongeza hatari ya vidonda na kuchelewesha kupona.


7. Ulaji wa vyakula vyenye pilipili kali, asidi nyingi, au vyakula vya kukaangwa.


BAADHI YA DALILI YA VIDONDA VYA TUMBO



1. Maumivu makali au ya kuchoma kwenye tumbo (hasa sehemu ya juu ya tumbo).


2. Maumivu huweza kuja ikiwa tumbo lipo tupu au baada ya kula na kushiba sana.


3. Kupata ganzi za mara kwa mara kwenye vidole, tumbo kujaa gesi, kupoteza hamu ya kula na kujihisi kichefuchefu.


4. Kutapika damu, kupungukiwa na damu lakini pia kuhisi kizunguzungu.


5. Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.


6. Kuvimba au kuhisi tumbo kujaa haraka.


7. Damu kwenye kinyesi (kinyesi cheusi) au kutapika damu ni dalili ya hatarishi.


BAADHI YA MADHARA YA VIDONDA SUGU VYA TUMBO



1. Chanzo cha saratani yani kansa ya utumbo mpana, ambayo pia husambaa hadi kwenye ini na kusababisha saratani ya ini kwa njia ya metastasis.


2. Kutoboka kwa ukuta wa tumbo (perforation) hatari kubwa inayohitaji upasuaji.


3. Kuvuja damu ndani ya mfumo wa mmeng'enyo


4. Kuzuia chakula kupita vizuri kutoka tumboni kwenda kwenye utumbo mdogo.


5. Kansa ya tumbo (kwa baadhi ya vidonda sugu vilivyodumu muda mrefu).


USHAURI NA MATIBABU



1. Tibu magonjwa ya ini kama tayari una matatizo ya ini, ili kuimarisha mfumo wa chakula na enzymes (vimeng'enya)


2. Mgonjwa hutumia dawa maalumu za kuua bakteria wa H. pylori (baktaria wa vidonda  vya tumbo)


3. Mgonjwa hutumia dawa za kupunguza na kuzuiya uzalishwaji wa  asidi tumboni 


4. Mgonjwa hutumia dawa za Antacids, dawa ambazo husaidia katika kupunguza na kuondoa maumivu ya tumbo na misuli.


5. Mgonjwa huudhulia dozi ya kuondoa vichomi sugu, dalili za bawasili


6. Mgonjwa hutumia dawa za kuondoa ganzi na seli za kansa za utumbo mpana


7. Mgonjwa anashauriwa sana kuepuka dawa kali za hospitalini kama vile aspirin na NSAIDs.


8. Katika kipindi cha matibabu mgonjwa anapendekezwa kuweka mabadiliko ya lishe na maisha kwa ujumla ili kukidhi haja ya kutibu tatizo.


USHAURI..

- Epuka chakula chenye mafuta mengi na pilipili kali.


- Kula chakula kidogo kidogo mara kwa mara.


- Epuka kahawa, soda, na sigara.


- Usinywe pombe.


- Pata usingizi wa kutosha na epuka msongo wa mawazo.



Ukiona dalili zinazodumu kwa zaidi ya wiki moja au kutapika damu/kutoa damu kwenye kinyesi, muone daktari haraka kwa vipimo kama endoscopy, kipimo cha H. pylori, au ultrasound.

Ukihitaji matibabu salama ya vidonda vya tumbo na lishe bora kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo, karibu kwa huduma tunaweza kukusaidia zaidi.


KUMBUKA:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.

Karibu tukuhudumie, kwachangamoto za afya, tunatoa hudma ya VIPIMO, USHAURI na MATIBABU.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!