Kipimo cha kuangalia utendaji kazi wa ini
Liver Function Test (LFT) ni mfululizo wa vipimo vya damu vinavyopima jinsi ini linavyofanya kazi na hali yake kwa ujumla.
𝗟𝗜𝗩𝗘𝗥 𝗙𝗨𝗡𝗖𝗧𝗜𝗢𝗡 𝗧𝗘𝗦𝗧 (𝗞𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗞𝗨𝗔𝗡𝗚𝗔𝗟𝗜𝗔 𝗨𝗧𝗘𝗡𝗗𝗔𝗝𝗜 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗙𝗨𝗠𝗢 𝗪𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔
Vipimo hivi vinaangalia viwango vya 𝘃𝗶𝗺𝗲𝗻𝗴’𝗲𝗻𝘆𝗮 (𝗲𝗻𝘇𝘆𝗺𝗲𝘀), 𝗽𝗿𝗼𝘁𝗶𝗻𝗶, 𝗕𝗶𝗹𝗶𝗿𝘂𝗯𝗶𝗻, 𝗟𝗶𝗺𝗽𝗮𝘀𝗲, 𝗮𝗺𝗹𝘆𝘀𝗲, 𝗻𝗮 𝘁𝗮𝗸𝗮 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶𝗻𝗶 𝘃𝗶𝗻𝗮𝘃𝘆𝗼𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗮 𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗮𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶.
Hizi ni baadhi ya faida za kupima kipimo cha "Liver Function Test" (LFTs) — kipimo cha kuangalia utendaji kazi wa ini:
𝗞𝘂𝗯𝗮𝗶𝗻𝗶 𝗺𝗮𝗽𝗲𝗺𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝘃𝗶𝗹𝗲 𝗸𝘂𝘃𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶, 𝗰𝗶𝗿𝗿𝗵𝗼𝘀𝗶𝘀, 𝗻𝗮 𝘀𝗮𝗿𝗮𝘁𝗮𝗻𝗶 (𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗼𝗰𝗲𝗹𝗹𝘂𝗹𝗮𝗿 𝗰𝗮𝗿𝗰𝗶𝗻𝗼𝗺𝗮)
Liver Function test, husaidia kugundua matatizo ya ini kama hepatitis, uvimbe, cirrhosis, fatty liver, saratani ya ini na hata kabla ya dalili kuonekana wazi.
𝗞𝘂𝗳𝘂𝗮𝘁𝗶𝗹𝗶𝗮 𝗺𝗮𝗲𝗻𝗱𝗲𝗹𝗲𝗼 𝘆𝗮 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗻𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮
Kwa mgonjwa aliye tayari na tatizo la ini, vipimo hivi husaidia kujua kama ugonjwa unaendelea, umesimama au unaboreshwa na matibabu.
𝗞𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗮 𝗺𝗮𝗱𝗵𝗮𝗿𝗮 𝘆𝗮 𝗱𝗮𝘄𝗮, 𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗹𝗲 𝘄𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗕 𝗮𝘂 𝗖 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗼 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮𝗯𝘂
Baadhi ya dawa (kama za kifua kikuu au ARVs) zinaweza kuharibu ini. Kipimo cha ini huangalia kama ini linaathiriwa na dawa.
𝗞𝘂𝘀𝗮𝗶𝗱𝗶𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗱𝗮𝗹𝗶𝗹𝗶 𝘇𝗶𝘀𝗶𝘇𝗼𝗲𝗹𝗲𝘄𝗲𝗸𝗮 𝘇𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶
Dalili kama uchovu mkali, njaa ya mara kwa mara, kichefuchefu, manjano (jaundice), na maumivu ya tumbo huweza kuwa ni ishara za matatizo ya ini. Kipimo cha Liver functions husaidia kuchunguza chanzo cha tatizo inaweza kuwa maambukizi ya virus vya homa ya ini, sumu, pombe au minyoo ya kichocho.
𝗞𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗮 𝘂𝗳𝗮𝗻𝗶𝘀𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮𝗯𝘂 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗮𝘁𝘂𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶
Kwa mgonjwa anayetibiwa, LFTs husaidia kuthibitisha kama dawa au tiba inafanya kazi vizuri au la.
𝗞𝘂𝗴𝘂𝗻𝗱𝘂𝗮 𝘂𝗵𝗮𝗿𝗶𝗯𝗶𝗳𝘂 𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝘂𝘀𝗶𝗼 𝗻𝗮 𝗱𝗮𝗹𝗶𝗹𝗶
Watu wengi huishi na uharibifu wa ini bila dalili yoyote. Kipimo hiki kinaweza kugundua hali hiyo mapema.
𝗞𝗶𝗽𝗶𝗺𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗹𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗳𝘂𝗻𝗰𝘁𝗶𝗼𝗻, 𝗵𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗶 𝘀𝗲𝗵𝗲𝗺𝘂 𝘆𝗮 𝘂𝗰𝗵𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝗺𝗲𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲
LFTs hutumika pia kama kipimo cha kuchunguza magonjwa mengine kama kisukari, shinikizo la damu, au saratani ambazo huweza kuathiri ini.
𝗞𝘂𝗽𝗶𝗺𝗮 𝗸𝗮𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗸𝗮𝗯𝗹𝗮 𝘆𝗮 𝘂𝗽𝗮𝘀𝘂𝗮𝗷𝗶
Kabla ya kufanyiwa upasuaji mkubwa, LFTs hufanyika kuhakikisha ini linaweza kuhimili dawa za usingizi na tiba nyingine.
𝗞𝘂𝗽𝗶𝗺𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗼𝘁𝘂𝗺𝗶𝗮 𝗽𝗼𝗺𝗯𝗲 𝗮𝘂 𝗺𝗮𝗱𝗮𝘄𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗹𝗲𝘃𝘆𝗮
Wale wanaotumia pombe kwa muda mrefu au dawa za kulevya hupaswa kufanyiwa LFTs ili kuchunguza kama ini limeharibika.
𝗞𝘂𝘄𝗲𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗺𝗯𝘂𝗸𝘂𝗺𝗯𝘂 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶
Kuwa na vipimo vya mara kwa mara kunawezesha madaktari kufahamu na kufuatilia mabadiliko yoyote ya utendaji kazi wa ini kwa muda na mabadiliko katika matibabu.
𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:- Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.
𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.