Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Ugonjwa wa figo, visababishi, dalili, madhara na matibabu


Fikia huduma za matibabu kwa ugonjwa wa figo na mfumo wa mkojo

𝗔𝗙𝗬𝗔 𝗬𝗔 𝗙𝗜𝗚𝗢 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗬𝗔𝗡𝗔𝗬𝗢 𝗔𝗧𝗛𝗜𝗥𝗜 𝗨𝗧𝗘𝗡𝗗𝗔𝗝𝗜 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗙𝗜𝗚𝗢:

 

Figo (Kidney) Ni kiungo cha mwili ambacho kina jukumu la kuchuja damu na kuondoa taka mwilini kupitia mkojo.

Binadamu ana figo mbili, moja upande wa kushoto na nyingine upande wa kulia wa mgongo, chini ya mbavu.

 

 


𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗭𝗔 𝗙𝗜𝗚𝗢 𝗠𝗪𝗜𝗟𝗜𝗡𝗜:

Figo (kidney) zina kazi muhimu mwilini, zikiwemo:

 

✔️ 𝗞𝘂𝘀𝗮𝗳𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶𝗻𝗶:

Figo huondoa taka mwilini kama urea, creatinine, na asidi ya uric kupitia mkojo.

 

✔️ 𝗞𝘂𝗱𝗵𝗶𝗯𝗶𝘁𝗶 𝗸𝗶𝘄𝗮𝗻𝗴𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗺𝗮𝗷𝗶 𝗻𝗮 𝗰𝗵𝘂𝗺𝘃𝗶 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶𝗻𝗶:

Zinasaidia kuweka uwiano wa maji, sodiamu, na madini mengine ili mwili ufanye kazi vizuri.

 

✔️ 𝗞𝘂𝗱𝗵𝗶𝗯𝗶𝘁𝗶 𝘀𝗵𝗶𝗻𝗶𝗸𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂:

Figo huzalisha homoni (renin) inayosaidia kudhibiti shinikizo la damu.

 


 

✔️ 𝗞𝘂𝗰𝗵𝗼𝗰𝗵𝗲𝗮 𝘂𝘇𝗮𝗹𝗶𝘀𝗵𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝘀𝗲𝗹𝗶 𝗻𝘆𝗲𝗸𝘂𝗻𝗱𝘂 𝘇𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂:

Zinatoa homoni iitwayo erythropoietin (EPO), ambayo huchochea uboho wa mifupa kutengeneza seli nyekundu za damu.

 

✔️ 𝗞𝘂𝗱𝗵𝗶𝗯𝗶𝘁𝗶 𝗸𝗶𝘄𝗮𝗻𝗴𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗮𝘀𝗶𝗱𝗶 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶𝗻𝗶:

Figo zinahakikisha mwili unadumisha usawa wa asidi na besi (pH balance).

 

✔️ 𝗞𝘂𝗰𝗵𝘂𝗷𝗮 𝗱𝗮𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗲𝗺𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶 𝗵𝗮𝘁𝗮𝗿𝗶:

Zinasaidia kuondoa mabaki ya dawa na sumu mwilini.

 

✔️ 𝗞𝘂𝘁𝗲𝗻𝗴𝗲𝗻𝗲𝘇𝗮 𝗩𝗶𝘁𝗮𝗺𝗶𝗻𝗶 𝗗:

  • Figo hubadilisha vitamini D kuwa mfumo wake wa kazi, unaosaidia kunyonya kalsiamu kwa afya ya mifupa.

 

  • Figo zina jukumu kubwa la kuweka mwili katika hali ya usawa (homeostasis).

     

𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗩𝗜𝗦𝗔𝗕𝗔𝗕𝗜𝗦𝗛𝗜 𝗩𝗜𝗡𝗔𝗩𝗬𝗢 𝗔𝗧𝗛𝗜𝗥𝗜 𝗔𝗙𝗬𝗔 𝗬𝗔 𝗙𝗜𝗚𝗢:

Baadhi ya visababishi vya magonjwa ya figo ni vingi, na mara nyingi vinahusiana na maisha, lishe, na magonjwa mengine sugu:

 

✔️ 𝗠𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝗦𝘂𝗴𝘂 𝘆𝗮𝗻𝗮𝘆𝗼 𝗮𝘁𝗵𝗶𝗿𝗶 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗳𝗶𝗴𝗼:

Ugonjwa wa Tezi dume.

 



- Shinikizo la damu (Hypertension) – Husababisha uharibifu wa mishipa ya damu ya figo.

 - Kisukari (Diabetes) – Viwango vya juu vya sukari huharibu nephrons (seli za kuchuja damu kwenye figo).

 

✔️ 𝗠𝗮𝘁𝘂𝗺𝗶𝘇𝗶 𝗠𝗮𝗯𝗮𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗗𝗮𝘄𝗮:

 - Dawa za kutuliza maumivu (NSAIDs) kama ibuprofen na diclofenac kwa muda mrefu.

 - Dawa za antibayotiki zisizotumika kwa usahihi.

 

✔️ 𝗠𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗠𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗮𝘁𝗵𝗶𝗿𝗶 𝘂𝘄𝗲𝘇𝗼 𝘄𝗮 𝗞𝗶𝗻𝗴𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶:

- Maambukizi ya bakteria katika mfumo wa mkojo ambao pia huathiri kwenye figo (pyelonephritis), U.T.I na kichocho.

 - Magonjwa ya kuathiri mfumo wa kinga ya mwilini kama lupus, H.I.V, Hepatitis na Typhode.

 

 


✔️ 𝗠𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗞𝗶𝗷𝗲𝗻𝗲𝘁𝗶𝗸𝗶 𝗻𝗮 𝗞𝗶𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶:

- Magonjwa ya kurithi kama Polycystic Kidney Disease (PKD).

- Kuziba kwa mkojo kutokana na mawe kwenye figo au kibofu.

 

✔️ 𝗟𝗶𝘀𝗵𝗲 𝗻𝗮 𝗠𝘁𝗶𝗻𝗱𝗼 𝘄𝗮 𝗠𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮:

- Ulaji mwingi wa chumvi na vyakula vyenye mafuta mengi.

 - Kunywa pombe kupita kiasi na uvutaji sigara.

 - Kutokunywa maji ya kutosha.

 

✔️ 𝗠𝘀𝗼𝗻𝗴𝗼 𝘄𝗮 𝗠𝗼𝘆𝗼 𝗻𝗮 𝗞𝘂𝘇𝗲𝗲𝗸𝗮:

- Umri mkubwa huongeza hatari ya figo kushindwa kufanya kazi.

 - Magonjwa ya moyo yanaweza kuathiri mtiririko wa damu kwenda kwenye figo.

 

𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗕𝗢𝗥𝗔 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗗𝗛𝗜𝗕𝗜𝗧𝗜 𝗔𝗙𝗬𝗔 𝗬𝗔 𝗙𝗜𝗚𝗢:




Njia bora ya kuzuia magonjwa ya figo:

 

✔️ Dhibiti afya ya Tezi dume na kibofu.

 

✔️ Kudhibiti shinikizo la damu.

 

✔️ Kudhibiti ugonjwa wa kisukari.

 

✔️ Kubadili mtindo wa maisha katika lishe, kula lishe bora.

 

✔️ kunywa maji ya kutosha, na kuepuka dawa zinazoweza kuathiri figo.

 

✔️ Tibu au dhibiti magonjwa ya kuambukiza.

 

✔️ Hepuka ngono zembe ambayo huchochea kupata magonjwa ya kuambukiza kama vile U.T.I, kichocho, Gonorrhoea, Hepatitis na H.I.V.

 

 

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.

 

𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!