Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Jamii ya vyakula vyenye protini nyingi - Vinaweza kuwa hatari kwa ini


Orodha ya vyakula vyenye protini nyingi vilivyogawanywa katika makundi mawili: vya asili ya wanyama (animal-based) na asili ya mimea (plant-based):


Vyakula vya asili ya wanyama vyenye protini nyingi

1. Nyama ya ng'ombe (beef)

 

2. Kuku (chicken) hasa kifua cha kuku au kidali

 

3. Samaki hasa tuna, salmon, dagaa, mackerel

 

4. Mayai hasa yai zima (kiini na ute)

 

5. Maziwa fresh na mtindi

 


 

6. Jibini (cheese)  hasa cheddar, mozzarella, cottage cheese

 

7. Mtindi wenye protini nyingi (Greek yogurt)

 

8. Maini hasa maini ya kuku au ng'ombe

 

9. Viungo vya ndani kwa wanyama (organ meats) kama figo, moyo, na ini

 

10. Dagaa wa kukaanga au kukaushwa (full body protein)

 

Vyakula vya asili ya mimea vyenye protini nyingi (Plant Based Protein)

 



1. Maharagwe ya aina zote  (maharagwe mekundu, ya soya, n.k.)

 

2. Njugu mawe na karanga

 

3. Mbegu za maboga (pumpkin seeds)

 

4. Lentili (lentils)

 

5. Chickpeas (kunde au dengu kubwa)

 

6. Nazi (Nazi ina sifa ya kuwa na mafuta yemye amino acids)

 

7. Quinoa nafaka yenye protini kamili

 

8. Nyewele za shayiri na oats

 

9. Tofu na tempeh vyakula vilivyotokana na maharagwe ya soya

 

10. Mbegu za alizeti, chia na flaxseed

 

BAADHI YA VIDOKEZO MUHIMU

 



 

🔹 Vyakula vya asili ya wanyama vina protini kamili (full amino acid profile).

 

🔹 Wenye matatizo ya ini hawapaswi kula protini nyingi bila kushauriwa na daktari.

 

🔹 Kwa wagonjwa wa ini, protini bora ni zile nyepesi kusindika, kama dagaa, samaki wa kuchemsha, maharagwe yaliyopikwa vizuri, na mayai kwa kiasi.

 


 

 

KUMBUKA:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.

 

Karibu tukuhudumie, kwa changamoto za afya, tunatoa huduma za VIPIMO, MATIBABU, USHAURI na CHANJO

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!