Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Vyakula vilivyo chakatwa (Processed Foods) si salama kwa wagonjwa wa Ini, Kisukari, Figo, Presha na Saratani


Vyakula vilivyosindikwa nivyakula ambavyo vimebadilishwa kutoka hali yao ya asili, nzima, kuanzia vitu vilivyobadilishwa kidogo kama vile mboga zilizokatwa tayari hadi vyakula vilivyochakatwa kwa wingi kama vile chipsi na vinywaji vyenye sukari.

USILE VYAKULA VILIVYO CHAKATWA (PROCESSED FOODS)


Vyakula vilivyochakatwa (processed foods) ni vyakula ambavyo vimebadilishwa kutoka hali yake ya asili kupitia njia mbalimbali za viwandani au kiasilia ili viweze kudumu muda mrefu, kuonekana vizuri zaidi, au kuwa na ladha fulani.




ambavyo mara nyingi huwa na sukari iliyoongezwa , chumvi , mafuta na viambato bandia vya kuhifadhi, ladha au umbile. Ingawa usindikaji fulani unaweza kuboresha usalama na lishe, matumizi ya kupita kiasi ya vyakula vilivyochakatwa sana yanaweza kudhuru afya kutokana na viwango vya juu vya viungio visivyofaa


Mfano wa mchakato: 𝗸𝘂𝗸𝗮𝗮𝗻𝗴𝘄𝗮, 𝗸𝘂𝗸𝗮𝘂𝘀𝗵𝘄𝗮, 𝗸𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝘄𝗮 𝗰𝗵𝘂𝗺𝘃𝗶 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶, 𝘀𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶, 𝗺𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮, 𝘃𝗶𝗵𝗶𝗳𝗮𝗱𝗵𝗶 (𝗽𝗿𝗲𝘀𝗲𝗿𝘃𝗮𝘁𝗶𝘃𝗲𝘀), 𝗿𝗮𝗻𝗴𝗶 𝗯𝗮𝗻𝗱𝗶𝗮, 𝗮𝘂 𝗹𝗮𝗱𝗵𝗮 𝗯𝗮𝗻𝗱𝗶𝗮.


🔹 Mfano wa mchakato: kukaangwa, kukaushwa, kuongezwa chumvi nyingi, sukari, mafuta, vihifadhi (preservatives), rangi bandia, au ladha bandia.


Aina kuu za vyakula vilivyochakatwa


✔️ 𝗖𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗶𝗰𝗵𝗼𝗽𝗶𝗸𝘄𝗮 𝘁𝗮𝘆𝗮𝗿𝗶

Mfano: sausage, chipsi, samosa, mikate ya viwandani.


✔️ 𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝘃𝗶𝗹𝗶𝘃𝘆𝗼𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝘄𝗮 𝘃𝗶𝗵𝗶𝗳𝗮𝗱𝗵𝗶 𝗮𝘂 𝗹𝗮𝗱𝗵𝗮

Mfano: soda, juisi za pakiti, biskuti, peremende.


✔️ 𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝘃𝗶𝗹𝗶𝘃𝘆𝗼𝗽𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝘄𝗮 𝘃𝗶𝗿𝘂𝘁𝘂𝗯𝗶𝘀𝗵𝗼

 

Mfano: mchele mweupe uliosafishwa sana, unga wa ngano uliokobolewa.


✔️ 𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝘃𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗸𝗼𝗽𝗼 𝗮𝘂 𝗽𝗮𝗸𝗶𝘁𝗶 – mfano: nyama ya kopo, samaki wa kopo, supu za pakiti.

 

𝗞𝗜𝗡𝗬𝗨𝗠𝗘 𝗖𝗛𝗔𝗞𝗘:


  • Vyakula visivyochakatwa au asilia ni vile vinavyoliwa karibu na hali yake ya asili, mfano:

     

  • Matunda na mboga mbichi

     

  • Nafaka zisizokobolewa (kama ulezi, mtama, mchele wa kahawia)

     

  • Samaki au nyama mbichi isiyoongezwa kemikali

     

  • Maharage, dengu, kunde


𝗦𝗔𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗡𝗔 𝗦𝗔𝗥𝗔𝗧𝗔𝗡𝗜 𝗛𝗔𝗣𝗔𝗦𝗪𝗜 𝗞𝗨𝗧𝗨𝗠𝗜𝗔 𝗩𝗬𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔 𝗛𝗜𝗩𝗜:


Mgonjwa wa ini hashauliwi kutumia vyakula vilivyochakatwa (processed foods) kwa sababu kuu zifuatazo:


✔️ 𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝘃𝗶𝗹𝗶𝘃𝘆𝗼 𝗰𝗵𝗮𝗸𝗮𝘁𝘄𝗮 𝘃𝗶𝗻𝗮 𝘄𝗶𝗻𝗴𝗶 𝘄𝗮 𝗰𝗵𝘂𝗺𝘃𝗶 (𝘀𝗼𝗱𝗶𝘂𝗺):

Vyakula vilivyochakatwa mara nyingi vina chumvi nyingi, ambayo husababisha mwili kushikilia maji na kupelekea uvimbe (edema) na tumbo kujaa maji (ascites) kwa wagonjwa wa ini.

 

✔️ 𝗩𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝗵𝗶𝘃𝗶 𝘃𝗶𝗻𝗮 𝘄𝗶𝗻𝗴𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮 𝗺𝗮𝗯𝗮𝘆𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗲𝗺𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶:

Processed foods huwa na mafuta ya viwandani (trans fats, saturated fats) ambayo huongeza shinikizo kwa ini na kuharibu zaidi seli za ini.


✔️ 𝗦𝘂𝗺𝘂 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘇𝗼 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘁𝗼𝗸𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝗻𝗮𝗺𝗻𝗮 𝘃𝘆𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝗶𝘃𝘆𝗼 𝘃𝗶𝗹𝗶𝘃𝘆𝗼 𝘁𝗲𝗻𝗴𝗲𝗻𝗲𝘇𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗵𝘂𝗳𝗮𝗱𝗵𝗶𝘄𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝘂𝗱𝗮 𝗺𝗹𝗲𝗳𝘂 𝗸𝘂𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝗸𝗲𝗺𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝗰𝗮𝗿𝗯𝗼𝗻:


Ini ndiyo kiungo kinachosafisha na kuvunja sumu mwilini. Wagonjwa wa ini wakiwa na ini dhaifu, huathiriwa zaidi na kemikali hizi ambazo zinaweza kuongeza kasi ya kuharibika kwa ini.


✔️ 𝗩𝗶𝗻𝗮 𝘄𝗶𝗻𝗴𝗶 𝘄𝗮 𝗦𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗴𝗮 𝘃𝗶𝘁𝘂 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘃𝘆𝗼 𝗵𝘂𝗰𝗵𝗼𝗰𝗵𝗲𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗵𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝗺𝗳𝘂𝗺𝗼 𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮:

Vyakula vilivyochakatwa kama soda, biskuti, keki na juisi za viwandani huwa na sukari nyingi ambayo inaweza kusababisha mafuta kukusanyika kwenye ini (fatty liver) na kudhoofisha zaidi ini.


✔️ 𝗨𝗽𝘂𝗻𝗴𝘂𝗳𝘂 𝘄𝗮 𝘃𝗶𝗿𝘂𝘁𝘂𝗯𝗶𝘀𝗵𝗼 𝗵𝗮𝗹𝗶𝘀𝗶:

Processed foods mara nyingi hupoteza vitamini na madini muhimu. Wagonjwa wa ini wanahitaji chakula chenye virutubisho kamili ili kusaidia mwili na kinga yao.


𝗞𝘄𝗮 𝘂𝗳𝘂𝗽𝗶: Wagonjwa wa ini wanashauriwa kuepuka vyakula vilivyochakatwa kwa sababu 𝘃𝗶𝗻𝗮𝗰𝗵𝗼𝘀𝗵𝗮 𝗶𝗻𝗶, 𝘃𝗶𝗻𝗮𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝗵𝗮𝘁𝗮𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝘂𝘃𝗶𝗺𝗯𝗲 𝗻𝗮 𝘀𝘂𝗺𝘂, 𝗻𝗮 𝗵𝗮𝘃𝗶𝗻𝗮 𝘃𝗶𝗿𝘂𝘁𝘂𝗯𝗶𝘀𝗵𝗼 𝘃𝘆𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗼𝘀𝗵𝗮 𝗸𝘂𝘀𝗮𝗶𝗱𝗶𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶.

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨, 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜:

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!