Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Homa ya ini - hatua za ugonjwa wa ini, dalili, madhala, visababishi na matibabu


Kuishi na maambukizi ya virus vya homa ya ini (Hepatitis) sio sehemu ya maisha yako, hatua za ushindi katika kupona na kurejesha tumaini jipya la maisha yenye afya huanza na wewe mwenyewe leo


Hepatitis B ni virus vinavyo sababisha ugonjwa wa ini wa kuambukiza, kuna aina nyingi sana ya virus vya hepatitisi ambavyo husababisha ugonjwa wa ini na saratani (𝗠𝗳𝗮𝗻𝗼: 𝗵𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗔, 𝗕, 𝗖, 𝗗 𝗻𝗮 𝗘).

 

Hepatitis B, ni moja ya aina kuu ya virus vinavyo sababisha homa ya ini kali, na inaweza kusababisha maambukizi ya muda mfupi (acute infection) yasiyo hitaji matibabu ikaisha yenyewe kwa mfumo wa kinga kwa muda wa miezi mitatu (3) hadi sita (6) au maambukizi ya muda mrefu yenye kuhitaji matibabu madhubuti (mpango mkakati wa kitabibu) katika kupata suluhisho la kudumu au kutibu:

 

𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗭𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗕𝗨𝗞𝗜𝗭𝗜.𝗞𝗪𝗔 𝗩𝗜𝗥𝗨𝗦 𝗩𝗬𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗕


✔️ Kugusana na damu yenye virusi (mfano sindano, jeraha, transfusion isiyo salama).


✔️ Kujamiiana bila kinga na mtu mwenye virusi.


✔️ Mama mwenye HBV kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua.


✔️ Kutumia vifaa vya binafsi kwa pamoja (Nguo, Miswaki, Wembe na Sindano).


✔️ Kushika maji maji yenye virusi wa hbv yatokayo mwilini mwa mtu alie ambukizwa kama vile Jasho, mate, damu, machozi au manii.

 

𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗗𝗔𝗟𝗜𝗟𝗜 𝗭𝗔 𝗨𝗪𝗘𝗣𝗢 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗕𝗨𝗞𝗜𝗭𝗜 𝗬𝗔 𝗩𝗜𝗥𝗨𝗦 𝗕 𝗠𝗪𝗜𝗟𝗜𝗡𝗜:

Kwa mara ya kwanza watu wengi huambumbukizwa na baadhi yao huishi kwa miaka mingi bila kuwa na dalili za mapema.


Baadhi ya wagonjwa wanaweza kupitia changamoto mbali mbali za kiafya kama dalili za awali baada tu ya kuambukizwa:

Dalili tofauti tofauti zinaweza kujitokeza kwa wagonjwa endapo tatizo litaendelea kudumu kwa miaka mingi pasipo kutibiwa, kufuata kanuni sahihi za ushauri wa lishe yenye afya na vipimo vya mara kwa mara:


✔️ Vidonda sugu vya tumbo yani (kuharibika kwa mfumo wa chakula)


✔️ Tumbo kuhisi limejaa ukila kidogo umeshiba kutokana na uwepo wa gesi nyingi tumboni


✔️ Uchovu mkali, kichefuchefu, kutapika na kupoteza hamu ya kula.


✔️ Maumivu ya tumbo upande wa kulia chini ya mbavu (Eneo la ini)


✔️ Miwasho sugu ya ngozi inaweza kuwa asubui baada ya kuoga, mchana au usiku wakati wa kuvua nguo.


✔️ Kukojoa mkojo wa njano kali au kahawiya pindi tatizo litakapo endelea kuwepo zaidi siku hadi siku dalili hujitokeza za wazi wazi.


✔️ Kukonda na kupungua uzito kwa kasi.


✔️ Ngozi kuwa kavu na yenye athiri kama ya vipere vipere katika uso wa ngozi.


✔️ Msongo mkubwa wa mawazo na kuwa na nafsi ya unyonge yenye kupoteza matumaini ya kuishi (Kuzidi kwa hofu)


✔️ Kupungukiwa na damu kutoka na ukosefu wa virutubisho vya msingi mwilini pamoja na kasi ya uvunjwaji wa seli nyekundu za damu.


✔️ Kupumua kwa shida au kifua kubana.


✔️ Miguu kujaa maji (Edema)


✔️ Macho na ngozi kuwa ya njano (jaundice)


✔️ Tumbo kuvimba au kujaa maji (Ascites) final stage.


𝗛𝗔𝗧𝗨𝗔 𝗭𝗔 𝗨𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗕𝗨𝗞𝗜𝗭𝗜 𝗬𝗔 𝗩𝗜𝗥𝗨𝗦 𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦:

Ugonjwa wa ini (hasa unaosababishwa na virus vya hepatitis B na C huwa unaendelea hatua kwa hatua, na kama mgonjwa hatopata matibabu stahiki ya mapema, tatizo linaweza kuendelea siku hadi siku na kusababisha kansa au saratani ya ini.

Kwa kawaida madaktari huueleza kwa hatua tano kuu za maendeleo ya ugonjwa wa ini usio tibiwa na kufuatiliwa:


𝗛𝗮𝘁𝘂𝗮 𝟭: 𝗜𝗻𝗶 𝗟𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗔𝗳𝘆𝗮 (𝗛𝗲𝗮𝗹𝘁𝗵𝘆 𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿)


✔️ Ini hufanya kazi vizuri bila uharibifu wowote.


✔️ Hakuna dalili, ini linaweza kujisafisha na kurekebisha lenyewe kwa matatizo madogo Madogo.


✔️ Wagonjwa wengi hawana dalili yoyote na huwezi kuwatambua kama wana changamoto hii na hata wenyewe hawajifahamu mpaka pale watakapo pima.

 

𝗛𝗮𝘁𝘂𝗮 𝟮: 𝗨𝗰𝗵𝗼𝗰𝗵𝗲𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗜𝗻𝗶 (𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗜𝗻𝗳𝗹𝗮𝗺𝗺𝗮𝘁𝗶𝗼𝗻 – 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀)


✔️ Ini huanza kushambuliwa na virusi, pombe, au sumu.


✔️ Kinga ya mwili dhaifu na virus  husababisha uvimbe (inflammation).


𝗗𝗮𝗹𝗶𝗹𝗶 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗻𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗼𝗻𝗲𝗸𝗮𝗻𝗮: Uchovu, kichefuchefu, maumivu upande wa kulia, ngozi au macho kuwa ya njano (jaundice).

 

𝗛𝗮𝘁𝘂𝗮 𝟯: 𝗙𝗶𝗯𝗿𝗼𝘀𝗶𝘀 (𝗞𝘂𝘄𝗲𝗽𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝗠𝗮𝗸𝗼𝘃𝘂 𝘆𝗮 𝗔𝘄𝗮𝗹𝗶)


✔️ Uvimbe wa muda mrefu husababisha tishu za nyuzi (scar tissue) kuanza kuchukua nafasi ya tishu za kawaida za ini.


✔️ Ini bado linaweza kufanya kazi kwa sehemu, lakini linaanza kudhoofika.


✔️ Mara nyingi dalili ni chache ila ni kubwa na za kudumu.


𝗛𝗮𝘁𝘂𝗮 𝟰: 𝗖𝗶𝗿𝗿𝗵𝗼𝘀𝗶𝘀 (𝗜𝗻𝗶 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗼𝘃𝘂 𝗴𝘂𝗺𝘂)


✔️ Makovu yanakuwa mengi na kudumu (chronic scarring).

 

✔️ Mtiririko wa damu ndani ya ini hupungua, ini hushindwa kufanya kazi vizuri.


🔹𝗗𝗮𝗹𝗶𝗹𝗶 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘇𝗼 𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝗵𝗶𝗶 𝘆𝗮 𝗻𝗻𝗲 (𝟰)


✔️ Kujaa maji tumboni (ascites)


✔️ Miguu kuvimba


✔️ Macho na ngozi kuwa ya njano zaidi


✔️ Kubadilika kwa akili (hepatic encephalopathy)


✔️ Kutokwa damu kwa urahisi

 

𝗛𝗮𝘁𝘂𝗮 𝟱: 𝗦𝗮𝗿𝗮𝘁𝗮𝗻𝗶 𝘆𝗮 𝗜𝗻𝗶 (𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗼𝗰𝗲𝗹𝗹𝘂𝗹𝗮𝗿 𝗖𝗮𝗿𝗰𝗶𝗻𝗼𝗺𝗮) 𝗮𝘂 𝗜𝗻𝗶 𝗞𝘂𝘀𝗵𝗶𝗻𝗱𝘄𝗮 𝗞𝗮𝗯𝗶𝘀𝗮 (𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗙𝗮𝗶𝗹𝘂𝗿𝗲)


✔️ Hatua ya mwisho, ini linashindwa kabisa kufanya kazi (end-stage liver disease).


✔️ Wagonjwa huhitaji matibabu ya dharura kama 𝗸𝘂𝗽𝗮𝗻𝗱𝗶𝗸𝗶𝘇𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 (𝗹𝗶𝘃𝗲𝗿 𝘁𝗿𝗮𝗻𝘀𝗽𝗹𝗮𝗻𝘁).


✔️ Hatari kubwa ya kupata saratani ya ini.

 

𝗞𝗪𝗔𝗞𝗜𝗙𝗨𝗣𝗜:

Afya → Inflammation → Fibrosis → Cirrhosis → Liver Failure/Saratani

 

𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗗𝗛𝗔𝗥𝗔 𝗣𝗜𝗡𝗗𝗜 𝗜𝗦𝗜𝗣𝗢 𝗗𝗛𝗜𝗕𝗜𝗧𝗜𝗪𝗔 𝗔𝗨 𝗞𝗨𝗧𝗜𝗕𝗜𝗪𝗔:


Homa ya ini sugu (uvimbe mwenye ini ulio sababishwa na virus hepatitis) kama haito tibiwa


✔️ Cirrhosis (ini kuwa gumu kutokana na makovu)


✔️ Saratani ya ini (Hepatocellular carcinoma)

 

𝗨𝗖𝗛𝗨𝗡𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗔𝗨 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢 𝗩𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗔𝗠𝗕𝗨𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔 𝗨𝗠𝗘𝗔𝗠𝗕𝗨𝗞𝗜𝗭𝗪𝗔:


✔️ Vipimo vya damu kama HBsAg, HBeAg, Anti-HBc, Anti-HBs


✔️ Liver function tests (ALT, AST)


✔️ Ultrasound au biopsy ya ini (kuchunguza uharibifu).

 

𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗩𝗜𝗥𝗨𝗦 𝗩𝗬𝗔 𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦 𝗕:

Acute: Mara nyingi hakuna matibabu yoyote katika hatua hii ya maambukizi inaweza kupotea yenyewe,  lakini pia inaweza kutibiwa kwa muda mfupi na maambukizi huisha bila mgonjwa kuona dalili au kufuatiliwa.


Hepatitis ya muda mlefu hutibiwa kupitia dawa zenye uwezo wa kulinda ini kuharibiwa, kupandisha kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana, kuona maambukizi sugu (Matibabu yanaweza kuwa ya muda mlefu na yenye ghalama):

 

  • Hutumia dawa za kudhibiti virusi.

     

  • kuondoa virus au maambukizi kwenye muundo wao wa seli shina.

     

  • kurejesha seli za ini zilizo chakaa au kudhoofika kutona na uwepo wa maambukizi kwa muda mlefu, mafuta au sukari ya ziada.

     

  • Kuzuia uzalishwaji wa seli za saratani ya ini kutokana na sumu nyingi pamoja na maambukizi ya muda mlefu.

     

  • Kuondoa makovu kwenye utando wa ini yani scar tissues.

      

  • kuongeza hamu ya kula na kuimarisha mfumo wa chakula, kutibu na kudhibiti asidi ya tumbo na vidonda vya tumbo.


✔️ Ufuatiliaji wa afya ya ini mara kwa mara kwa vipimo vya (liver function).

 

𝗞𝗜𝗡𝗚𝗔 𝗗𝗛𝗜𝗗𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗕𝗨𝗞𝗜𝗭𝗜 𝗬𝗔 𝗩𝗜𝗥𝗨𝗦 𝗪𝗔 𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦 𝗕:

✔️ Chanjo ya Hepatitis B baada tu ya kupona na kuthibitika huna maambukizi (kinga ni salama na yenye ufanisi mkubwa).

 

✔️ Kuepuka kutumia sindano au vifaa vya sharps kwa pamoja.


✔️ Kufanya ngono salama au kuachana na ngono zembe.

 

✔️ Kuchunguza wajawazito na kuwapa kinga watoto wachanga mara tu baada ya kuzaliwa.

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨, 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜:

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!