Ugonjwa wa kuzidi kwa acid reflex - Chanzo, dalili, madhara na matibabu
Ugonjwa wa kuzidi kwa asidi (acid reflux) hujulikana pia kama GERD (Gastroesophageal Reflux Disease) kwa Kiingereza.
𝗨𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗭𝗜𝗗𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗖𝗜𝗗 𝗥𝗘𝗙𝗟𝗨𝗫 - 𝗙𝗜𝗞𝗜𝗔 𝗛𝗨𝗗𝗨𝗠𝗔 𝗭𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗪𝗔 𝗟𝗜𝗦𝗛𝗘:
Huu ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mtu hupata changamoto ya vidonda vya tumbo kwa muda mlefu ambavyo visipo tibiwa husababisha kuzalishwa kwa asidi ya tumbo ambayo ikizidi asidi hii ya tumbo hupanda juu hadi kwenye mrija wa chakula (esophagus), na kusababisha maumivu makali ya kifua (heartburn) au hisia ya kuchoma.
𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗦𝗔𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗭𝗜𝗗𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗦𝗜𝗗 (𝗔𝗖𝗜𝗗 𝗥𝗘𝗙𝗟𝗨𝗫) 𝗧𝗨𝗠𝗕𝗢𝗡𝗜:
1. Kulegea kwa valve ya esophagus (LES) – Kipandikizi cha misuli (LES) kinaposhindwa kufunga vizuri, huruhusu asidi kurudi juu.
2. Kula chakula kingi sana mara moja.
3. Uzito mkubwa/obesity – huchochea presha tumboni.
4. Kula kabla ya kulala – huongeza uwezekano wa asidi kupanda.
5. Vyakula fulani – kama vyenye pilipili, limao, pombe, soda, kahawa, vyakula vya kukaangwa n.k.
6. Kuvuta sigara – huathiri LES.
7. Matumizi ya dawa kama NSAIDs (mfano: aspirin, ibuprofen).
8. Msongo wa mawazo (stress) – huongeza asidi tumboni.
𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗗𝗔𝗟𝗜𝗟𝗜 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗭𝗜𝗗𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗖𝗜𝗗 𝗥𝗘𝗙𝗟𝗨𝗫:
Hisia ya kuchoma choma kifuani kama kiungulia (heartburn).
Kuongezeka kwa mate mdomoni.
Kusikia uchachu au ladha ya asidi mdomoni na kooni
Maumivu ya koo au sauti kuwa chafu.
Kikohozi kikavu hasa usiku
Kuumwa na koo mara kwa mara bila sababu ya msingi.
Maumivu ya kifua yanayofanana na ya moyo.
- Ugumu wa kumeza chakula.
𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗗𝗛𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗨𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗔𝗖𝗜𝗗 𝗥𝗘𝗙𝗟𝗨𝗫:
Vidonda kwenye mrija wa chakula (esophageal ulcers).
Kubadilika kwa seli za esophagus (Barrett's esophagus) – huongeza hatari ya saratani
Kupungua uzito au upungufu wa damu kutokana na vidonda.
- Kukosa usingizi kutokana na maumivu ya usiku.
𝗡𝗔𝗠𝗡𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗞𝗜𝗡𝗚𝗔 𝗡𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗜𝗕𝗨 𝗨𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗭𝗜𝗗𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗖𝗜𝗗 𝗥𝗘𝗙𝗟𝗨𝗫:
Mabadiliko ya mtindo wa maisha na matibabu salama:
1. Tibu vidonda vya tumbo na magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile ini, bandama au nyongo kama una matatizo ayo.
2. Epuka vyakula vya kuchochea asidi.
3. Kula chakula kidogo kidogo lakini mara nyingi.
4. Epuka kuvaa nguo zinazobana tumbo.
5. Punguza uzito kama una uzito mkubwa.
6. Kunywa maji ya kutosha.
7. Epuka uvutaji wa sigara na pombe.
8. Epuka kulala mara baada ya kula (subiri angalau saa 2-3).
𝗗𝗔𝗪𝗔 𝗭𝗜𝗡𝗔𝗭𝗢 𝗧𝗨𝗠𝗜𝗞𝗔, 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗜𝗕𝗨 𝗨𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗭𝗜𝗗𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗦𝗜𝗗 𝗬𝗔 𝗥𝗘𝗙𝗟𝗨𝗫:
Dawa za kutibu vidonda vya tumbo, kuondoa choo kigumu na kuongeza hamu ya kula.
Dawa za kuondoa na kuzuiya ganzi pamoja na miguu kuuma au kuhisi hali ya fukuto
Kutibu na kuzuiya ugonjwa wa gout unao sababishwa na kuzidi kwa asid
Antacids, hizi ni dawa za kuondoa madhara ya asidi na kubalance kiwango sahihi cha asidi ya damu
Dawa za kuzuiya asidi kupanda na kuhisi hali ya kukereketa kwenye koo.
- Dawa za kuzuiya hali ya viungulia na kuhisi kichefuchefu.
- Dawa za kuongeza uwezo wa kusukuma chakula (prokinetics).
𝗠𝗨𝗛𝗜𝗠𝗨..:
Ikiwa unapata dalili mara kwa mara (zaidi ya mara 2 kwa wiki), unapaswa kumuona daktari. Kipimo cha endoscopy kinaweza kufanyika kuangalia hali ya esophagus kama kuna madhara.
Ukihitaji lishe bora na matibabu salama kwa mgonjwa mwenye changamoto ya kuzidi kwa asidi reflex, karibu sana kwa huduma za matibabu.
𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:- Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.
𝗠𝗔𝗛𝗔𝗟𝗜 𝗧𝗨𝗟𝗜𝗣𝗢: Hospitali, tunapatikana Dar es salaam Mbezi luis jirani na stendi kuu.
𝗛𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗺𝘂𝗼𝗻𝗮 𝗗𝗮𝗸𝘁𝗮𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝘂𝘀𝗵𝗮𝘂𝗿𝗶 𝗵𝘂𝘁𝗼𝗹𝗲𝘄𝗮 𝗯𝘂𝗿𝗲𝗲.
Unaweza kuwasiliana nasi kwakupiga simu au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia WhatsApp: +255628361104 +255746484873
𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨, 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜: