Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Mkojo wenye rangi ya njano, mwekundu na kahawia.


Mkojo ni kioevu kinachozalishwa na figo na kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo. Ni njia kuu ya mwili kujiondoa na kusafisha taka kama vile (Sumu, Mafuta, Protini na Acid) kutoka kwenye damu.

Kukojoa mkojo wa giza kama vile mkojo wenye rangi ya (Kahawia, njano iliyo kolea au hata rangi ya chai) kunaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ya kawaida au yasiyo ya kawaida yani (changamoto za kiafya). Hapa chini ni baadhi ya sababu kuu zinazo weza kusababisha hali iyo:


SABABU ZA KIAFYA ZINAZO HITAJI, UCHUNGUZI WA VIPIMO



 

Ukijihisi una tatizo moja wapo kati ya visababishi hivi, na unapata hali tofauti ya rangi ya mkojo basi jitahidi kufanya vipimo na matibabu ya mapema:


Maambukizi ya muda mrefu ya viru vya homa ya ini (Hepatitis A, B, C au D)

Inasababisha mkojo wa wenye rangi ya njano iliyo kolea au rangi ya giza kutokana na uwepo wa maambukizi hayo ya hepatitis B ambayo huchangia kuharibika kwa ini.


Matatizo ya magonjwa ya muda mrefu ya ini au figo hata bandama na kongosho




Kama hatua ya ini ya liver cirrhosis, hatua sugu ya ugonjwa wa figo tani kidney leptospirosis au liver failure, magonjwa haya huathiri usafishaji wa sumu mwilini


Uvimbe wa njia ya mkojo

Hii inaweza kuambatana na maumivu makali wakati wa kukojoa.


Kuvunjika kwa seli nyekundu za damu kwa wingi (Hemolysis)

Hii huachilia “Hemoglobin” kwenye mkojo na kuufanya kuwa mweusi au mwekundu.


Ugonjwa wa sickle cell anemia au malaria kali

Hali hizi huweza kusababisha uharibifu wa chembe hai za damu, na kutoa mkojo mweusi.


Maambukizi ya muda mrefu ya njia ya mkojo (U.T.I)

Mgonjwa mwenye maambukizi ya njia ya mkojo mara nyingi sana huambatana na mkojo wenye giza, harufu kali, na maumivu.


Mawe kwenye figo au maji (Kidney crystals)



 

Changamato hizi za figo zinapo dumu kwa muda mlefu, haja ndogo ya mgonjwa huambatana na damu au mkojo wa giza, na maumivu ya mgongo au tumbo.


BAADHI YA SABABU ZA KAWAIDA ZINAZO SABABISHA MABADILIKO YA RANGI YA MKOJO

▪️Upungufu wa maji mwilini (dehydration):


Ukikosa kunywa maji ya kutosha, mkojo huwa wa rangi ya njano iliyokolea au kahawia.


▪️Kula vyakula vyenye rangi kali:

Kama beetroot, karoti nyingi, au vyakula vyenye rangi ya bandia vinaweza kubadilisha rangi ya mkojo.


▪️Matumizi makubwa ya dawa fulani:

Kama vile dawa za malaria, dawa za maumivu (NSAIDs), au baadhi ya antibiotics (kama metronidazole, nitrofurantoin) zinaweza kubadilisha rangi ya mkojo.


🔎 UNATAKIWA KUFANYA NINI


▪️Kunywa maji mengi kwa siku moja hadi mbili. Kama mkojo hauko kawaida bado:


▪️Tembelea kituo cha afya kwa vipimo (kama vile urinalysis, liver/kidney function tests).


▪️Angalia dalili nyingine: kama njano ya macho/ngozi, maumivu, homa, au uchovu.




KUMBUKA:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


Karibu tukuhudumie, kwa changamoto za afya, tunatoa huduma za VIPIMO, MATIBABU, USHAURI na CHANJO

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!