Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Ugonjwa wa tezi dume, Dalili, Visababishi, Madhara na Matibabu


Zingatia ugonjwa wa tezi dume, pima afya yako ni ugonjwa ambao husababisha saratani ya tezi ya uzazi tezi dume na ugonjwa sugu wa figo


Tezi dume ni nini?


Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza  majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo. Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi.

Ipo wapi?


Tezi dume iko mwishoni mwa kibofu cha mkojo. Pia inauzunguks mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na na mrija wa mkojo  wa uume (urethra) na iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya fupa la nyonga.


Visababishi hatarishi vya Tezi dume


  • Umri  Mkubwa  kuanzia miaka 50


  • Vinasaba (ukoo wenye historia a saratani hii


  • Lishe hatarishi-nyama nyekundu kwa wingi, mafuta/samli,maziwa ya krimu


  • Unene uliokithiri


  • Ukosefu wa mazoezi


  • Upungufu wa virutubisho,mfano vit D.


  • Maambukizi ya mara kwa mara kwenye mfumo wa mkojo na tezi dume


Dalili zake ni zipi?


  • Udhaifu katika utoaji wa mkojo, mkojo hauishi.


  • Kwenda kukojoa mara kwa mara.

     

  •  Damu ndani ya mkojo.

     

  • Kushindwa kukojoa.

     

  • Maumivu ya kiuno na mifupa ya nyonga.

     

  • Wagonjwa wengi huanza maumivu ya nyonga kama ni dalili za awali.

     

  • Udhaifu katika utoaji wa mkojo pia kunaweza kutokea kwa kuvimba kwa tezi dume bila ya saratani.

     

  • Damu kwenye mkojo nakushindwa kumaliza mkojo ni ishara tosha ya kuwa  tezi dume imeathirika.

     

UCHUNGUZI


Wanaume wote wanpaswa kufanya uchunguzi wa tezi dume kuanzia miaka 50. Kwa wale wenye historia katika familia wanapaswa kuanza wakiwa na umri wa miaka 45.


  • Uchunguzi unafanyika kwa njia zifuatazo


  • Uchunguzi kwa cancer marker kwa kuchunguza damu (PSA).


  • Uchunguzi kwa njia ya kipimo cha njia ya haja kubwa (DRE)

     

  • Biopsy.

     

  • Ultrasound.

     

  • X-ray.

     

  • Bone scan.

 

Jinsi ya kutibu tezi dume


  • Dawa za kuondoa na kuzuia kuvimba na kutanuka kwa tezi dume


  • Dawa za kuimarisha afya ya figo na kibofu


  • Dawa za kuimarisha mfumo wa uzazi na nguvu za kiume


  • Dawa za kuondoa na kuzuia maumivu wakati wa kukojoa


Ugonjwa unapo kuwa mkubwa hatua za ziada za matibabu yanaweza kuchukuliwa


  • Upasuaji.

     

  • Mionzi

     

  • Homoni.

     

Matibabu hutegemea


  • Hatua ya ugonjwa ulipo fikia na afya ya mgonjwa.


  • Je, ugonjwa upo ndani ya tezi dume tu au umesambaa.

     

  • Umri na afya ya mgonjwa.

     

  • Magonjwa ambatanishi na tezi dume, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kisukari.


 


𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!