Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Kuzidi kwa kiwango cha protein mwilini (Protein overload)


Kiwango sahihi cha protini kinachohitajika mwilini hutegemea mambo kama vile:

✔️ Umri


✔️ Uzito wa mwili


✔️ Jinsia


✔️ Kiwango cha shughuli za mwili (mfano: kazi nzito au mkaaji)


✔️ Hali ya afya (kama ujauzito, magonjwa kama ugonjwa wa ini, figo n.k.)


 


Kiwango cha protini cha kawaida cha mtu mzima mwenye afya:


✔️  0.8 gramu za protini kwa kila kilo 1 ya uzito wa mwili kwa siku


MFANO:

Kama una uzito wa 60 kg, unahitaji kufanya calculation hii: 60 kg x 0.8 g = 48 gramu za protini kwa siku ambazo unahitaji uzipate pasipo kuzidi wala kupungua

 

Kiwango sahihi cha protini kwa  makundi mbali mbali:

Kundi la Watu Kiwango cha Protini (kwa kilo ya uzito)

✔️ Mtu mzima wa kawaida 0.8 g/kg. 


✔️ Mwanamichezo (anaye jenga misuli) 1.2-2.0 g/kg.


✔️ Mwanamke mjamzito 1.1-1.5 g/kg.


✔️ Wazee 1.0-1.2 g/kg.


✔️ Mgonjwa wa ini (kulingana na hali) Hupunguzwa hadi 0.6-0.8 g/kg.


✔️ Kuzidi kwa protini mwilini kwa mgonjwa wa ini na mfumo wa chakula:


Kuzidi kwa protini mwilini (protein overload) kwa kawaida haisababishi moja kwa moja homa ya ini (hepatitis) kama inavyo semekana.


Lakini inaweza kuathiri ini au kuongeza mzigo kwenye ini, hasa kama ini tayari lina changamoto au lina ugonjwa wa muda mlefu au miaka mingi bila kutibiwa.


Hapa chini ni baadhi zinazoeleza jinsi kuzidi kwa protini mwilini kunaweza kuathiri ini na kuchangia matatizo yanayofanana na homa ya ini na saratani au cirrhosis ya ini:



 

✔️ Husababisha mzigo mkubwa kwenye ini katika kusindika protini huhusika katika kuvunjavunja (metabolism) ya protini. 


Ini huhusika katika kuvunjavunja (metabolism) ya protini. Protini nyingi huongeza kazi ya ini, jambo linaloweza kuchangia uchovu wa ini au uharibifu wa seli zake kwa muda. Protini nyingi huongeza kazi ya ini, jambo linaloweza kuchangia uchovu wa ini au uharibifu wa seli zake kwa muda.


✔️ Kuongezeka kwa sumu nyingi mwilini yani Toksini (Ammonia)

Protini nyingi husababisha uzalishaji mwingi wa amonia (sumu), ambayo hutengenezwa wakati wa kuvunjwa kwa protini. Ikiwa ini limeathirika, halitaweza kusafisha amonia ipasavyo.


✔️ Ulaji wa protini kupita kiasi, husababisha hatari ya hepatic Encephalopathy


Kwa watu wenye ini dhaifu, ammonia ikizidi inaweza kuingia kwenye ubongo na kusababisha mabadiliko ya akili au kuchanganyikiwa (hepatic encephalopathy).


✔️ Kuzidi kwa protini nyingi mwilini, husababisha ahli ya shinikizo kwa ini ambalo tayari lina maambukizo na ugonjwa wa awali


Ikiwa mtu ana hepatitis sugu, protini nyingi zinaweza kuongeza mkazo kwa ini linalojaribu kupona au kupambana na maambukizi.


✔️ Protini nyingi husababisha ahli ya ini kuvimba (Liver inflammation)


Protini nyingi zinaweza kuchochea uzalishaji wa kemikali za uchochezi (inflammatory cytokines), na kuongeza hatari ya uvimbe kwenye ini.


✔️ Wingi wa protini kwenye damu, husababisha kuongezeka kwa homocysteine


Kiwango kikubwa cha protini fulani, hasa zinazotokana na wanyama, huongeza homocysteine, ambayo huhusishwa na madhara ya ini na moyo.


✔️ Protini kupita kiasi kwenye ini, husababisha ugonjwa wa ini wa mafuta tani Fatty liver disease


Protini nyingi kwenye mlo bila uwiano na wanga na mafuta, huweza kusababisha mkusanyiko wa mafuta kwenye ini (non-alcoholic fatty liver disease - NAFLD).


✔️ Protini inaweza kusababisha ahli ya ukinzani na baadhi ya viungo kama figo na ini katika kusafisha damu na sumu mwilini


Protini nyingi huweza kupunguza ufanisi wa ini katika kusafisha sumu mwilini, hasa kwa wagonjwa wa ini.


✔️ Protini husababisha au huchochea ahli ya maumivu ya tumbo hasa upande wa kulia wa tumbo


Kwa watu wenye ini linaloelemewa, wanaweza kuhisi maumivu au usumbufu upande wa juu kulia mwa tumbo, dalili inayofanana na homa ya ini.


✔️ Protini napo zidi kiwango, inaweza kuathiri ufanisi wa dawa katika matibabu


Protini nyingi zinaweza kuingiliana na utendaji kazi wa dawa za homa ya ini, au kubadilisha kasi ya dawa kusindika kwenye ini.


MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA LISHE SALAMA YA INI NA MFUMO WA CHAKULA


✔️ Kwa watu wenye ini lenye afya, kula protini nyingi haitasababisha homa ya ini moja kwa moja.


✔️ Kwa wenye magonjwa ya ini, kama hepatitis B/C au cirrhosis, mlo wenye protini nyingi haupendekezwi bila ushauri sahihi wa lishe kutokana na afya yako.


✔️ Protini nyingi kupita kiasi zinaweza kuchosha ini na figo, hasa kwa wagonjwa wa ini.

 

✔️ Protini chache sana huweza kuleta udhaifu, kupoteza misuli na kudhoofisha kinga ya mwili.


✔️ Bora kula protini kutoka vyanzo mbalimbali (wanyama na mimea) ili kupata asidi amino zote muhimu.


KUMBUKA:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.

 

Karibu tukuhudumie, kwa changamoto za afya, tunatoa huduma za VIPIMO, MATIBABU, USHAURI na CHANJO

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!