Chanjo ya homa ya ini - namna ya kuchoma na umuhimu wake
Hakikisha unachoma chanjo ya homa ya ini baada tu ya kupona, kwani nimuhimu sana ili kujikinga na maambukizi mapya
𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢 𝗬𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗕 - 𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦 𝗕 𝗩𝗔𝗖𝗖𝗜𝗡𝗔𝗧𝗜𝗢𝗡:
Chanjo ya homa ya ini (𝗵𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗕 𝘃𝗮𝗰𝗰𝗶𝗻𝗲) ni kinga muhimu inayotolewa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya homa ya ini B (HBV) kwa mtu asie na maambukizi au alie pona.
Muhimu kufahamu kuhusu chanjo ya homa ya ini:
✔️ 𝗔𝗶𝗻𝗮 𝘆𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶
Ni chanjo ya protini (HBsAg – sehemu ya uso wa virusi) ambayo hutengenezwa kwa teknolojia ya 𝗿𝗲𝗰𝗼𝗺𝗯𝗶𝗻𝗮𝗻𝘁 𝗗𝗡𝗔.
- Haina virusi hai, hivyo haiwezi kusababisha maambukizi.
𝟮. 𝗥𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮 𝘆𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 (𝗡𝗮𝗺𝗻𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗰𝗵𝗼𝗺𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼)
Kwa watoto wachanga: dozi ya kwanza hutolewa ndani ya saa 24 baada ya kuzaliwa, kisha dozi zingine 2–3 (kawaida jumla ya dozi 3 au 4).
- Kwa watu wazima: huchomwa dozi 3 kwa mpangilio wa miezi 0, 1, na 6.
✔️ 𝗨𝗳𝗮𝗻𝗶𝘀𝗶 𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶
Ina ufanisi mkubwa (95%+) ikiwa imechomwa kwa ratiba sahihi.
- Kinga inaweza kudumu zaidi ya miaka 20, na mara nyingi huchukuliwa kama ya kudumu maisha yote.
✔️ 𝗙𝗮𝗶𝗱𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝗼 𝘆𝗮 𝗵𝗼𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶
Inazuia maambukizi ya hepatitis B, ambayo husababisha matatizo makubwa kama cirrhosis na saratan ya ini (hepatocellular carcinoma) pindi isipo tibiwa.
- Pia hupunguza uwezekano wa kueneza HBV kutoka mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.
✔️ 𝗪𝗮𝗻𝗮𝗼𝗽𝗮𝘀𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗰𝗵𝗮𝗻𝗷𝘄𝗮
Watoto wachanga wote.
Watu wazima ambao hawajawahi kuchanjwa na wako kwenye hatari zaidi, mfano:
Wafanyakazi wa afya.
Wanaoishi au kuwa karibu na wagonjwa wa HBV.
Wanaotumia damu/dawa kwa sindano.
Wanaofanya ngono bila kinga mara kwa mara.
- Waliopona kutoka katika kuishi na maambukizi ya virus vya homa ya ini B
✔️ 𝗠𝗮𝗱𝗵𝗮𝗿𝗮 𝗺𝗮𝗱𝗼𝗴𝗼 𝘆𝗮𝗻𝗮𝘆𝗼𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮
Maumivu au uvimbe sehemu iliyodungwa sindano.
Homa ndogo au uchovu kwa muda mfupi.
- Athari kali sana ni nadra.
𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:- Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.
𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨, 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜: