Tafuta

Appointiment


*

Afya ya Ini - Usinywe soda wala kula vyakuala vilivyo sindikwa viwandani hasa viwanda vya kemikali


Matumizi ya Soda, vyakula vya kukaangwa na pombe kupita kiasi kwa mgonjwa wa homa ya ini, ni hatari sana kwa maendelo ya afya yako

𝗠𝗔𝗗𝗛𝗔𝗥𝗔  𝗬𝗔 𝗩𝗬𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔 𝗩𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗦𝗜𝗡𝗗𝗜𝗞𝗪𝗔 - 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗙𝗬𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗙𝗨𝗠𝗢 𝗪𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔:


Vyakula vya kusindikwa ni vyakula ambavyo vimepitia mchakato wa kubadilishwa kutoka hali yake ya asili kupitia njia kama vile:

 

𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗭𝗜𝗡𝗔𝗭𝗢 𝗧𝗨𝗠𝗜𝗞𝗔 𝗞𝗨𝗦𝗜𝗡𝗗𝗜𝗞𝗔 𝗩𝗬𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔:

 

  • Kupikwa na au kuokwa na kuongezwa rangi bandia.

     

  • Kukaushwa na joto ambalo sio la asili.

     

  • Kugandishwa kwa kemikali.

     

  • Kuongezwa viambato kama chumvi, sukari, mafuta au vihifadhi.

     

  • Kufungashwa kwenye makopo au plastiki kwa matumizi ya muda mrefu.

 

𝗠𝗙𝗔𝗡𝗢 𝗪𝗔 𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗩𝗬𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔 𝗩𝗜𝗟𝗜𝗩𝗬𝗢 𝗦𝗜𝗡𝗗𝗜𝗞𝗪𝗔:

 

  • Nyama za makopo au soseji (kama vienna, corned beef)

     

  • Vinywaji vya soda na juisi zilizosindikwa

     

  • Mikate ya viwandani

     

  • Biskuti na vitafunwa vya viwandani

     

  • Mchele ulioboreshwa au wali wa haraka (instant rice)

     

  • Supu za unga (instant soup).

     

  • Pombe na Chipsi za paketi.

 

𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗗𝗛𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗩𝗬𝗔𝗞𝗨𝗟𝗔 𝗩𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗦𝗜𝗡𝗗𝗜𝗞𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗔𝗙𝗬𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜:

 

Vyakula vya kusindikwa vinaweza kuwa na madhara kadhaa kwa afya ya ini, hasa ikiwa vinatumiwa kwa kiasi kikubwa na kwa muda mrefu.


𝗞𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗲𝗸𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗶𝗻𝗶 (𝗙𝗮𝘁𝘁𝘆 𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿):

 

Vyakula vya kusindikwa mara nyingi vina mafuta mengi yasiyo mazuri (𝗵𝗮𝘀𝗮 𝘁𝗿𝗮𝗻𝘀 𝗳𝗮𝘁𝘀), 𝘀𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶, 𝗻𝗮 𝗸𝗮𝗹𝗼𝗿𝗶 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶. Hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa mafuta kwenye ini (non-alcoholic fatty liver disease - NAFLD).


𝗠𝘀𝗼𝗻𝗴𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 (𝗟𝗶𝘃𝗲𝗿 𝘀𝘁𝗿𝗲𝘀𝘀):

 

Ini hufanya kazi ya kuchuja sumu mwilini. Vyakula vya kusindikwa vina viambata kama vihifadhi, 𝗿𝗮𝗻𝗴𝗶 𝗯𝗮𝗻𝗱𝗶𝗮, 𝗻𝗮 𝘃𝗶𝘂𝗻𝗴𝗶𝗼 𝘃𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝘃𝘆𝗮 𝗸𝗲𝗺𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶 ambavyo vinaweza kuchosha ini kwa muda mrefu.


𝗞𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗲𝗸𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗵𝗮𝘁𝗮𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘀𝘂𝗴𝘂 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶:

 

Ulaji wa mara kwa mara wa vyakula vya kusindikwa umehusishwa na kuongezeka kwa hatari ya magonjwa sugu ya ini kama 𝗰𝗶𝗿𝗿𝗵𝗼𝘀𝗶𝘀 na 𝗵𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗶𝘀𝗶𝘆𝗼 𝘆𝗮 𝘃𝗶𝗿𝘂𝘀𝗶, hasa pale mtu anapokuwa na mtindo mbaya wa maisha.


𝗞𝘂𝗽𝘂𝗻𝗴𝘂𝘇𝗮 𝘂𝘄𝗲𝘇𝗼 𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝘄𝗮 𝗸𝘂𝘀𝗮𝗳𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂:

 

Vyakula vyenye chumvi nyingi (kama vile nyama za kusindikwa) vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu kwenye ini (𝗽𝗼𝗿𝘁𝗮𝗹 𝗵𝘆𝗽𝗲𝗿𝘁𝗲𝗻𝘀𝗶𝗼𝗻), na pia kusababisha maji kujikusanya tumboni (𝗮𝘀𝗰𝗶𝘁𝗲𝘀), hali inayohusiana na ini dhaifu.


𝗞𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗲𝗸𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝘂𝘇𝗶𝘁𝗼 𝗸𝘂𝗽𝗶𝘁𝗮 𝗸𝗶𝗮𝘀𝗶 𝗻𝗮 𝗸𝗶𝘀𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶.

 

Vyakula hivi vinaweza kusababisha 𝘂𝘇𝗶𝘁𝗼 𝗸𝘂𝗽𝗶𝘁𝗮 𝗸𝗶𝗮𝘀𝗶 𝗻𝗮 𝗸𝗶𝘀𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶 𝗮𝗶𝗻𝗮 𝘆𝗮 𝟮, ambavyo vyote vina madhara ya moja kwa moja kwenye afya ya ini.


𝗡𝗢𝗧𝗘: Si vyakula vyote vya kusindikwa ni vibaya kiafya, lakini vile vilivyoongezwa sukari nyingi, chumvi nyingi au mafuta mabaya vinaweza kuwa hatari kwa afya ikiwa vitatumiwa kupita kiasi.

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!