Fahamu kuhusu homa ya ini na virus vya Hepatitis (A, B, C, D na E)
Kuna aina 5 kuu za virusi vya homa ya ini, inayojulikana kama aina A, B, C, D na E. Ingawa zote zinaweza kusababisha ugonjwa wa ini, zinatofautiana katika njia muhimu ikiwa ni pamoja na njia za maambukizi, ukali wa ugonjwa, usambazaji wa kijiografia, Matibabu na njia za kuzuia.
Hepatitis (kwa Kiswahili: homa ya ini) ni uvimbe au maambukizi katika ini, yanayosababishwa mara nyingi na virusi, lakini pia yanaweza kusababishwa na dawa, pombe, sumu, au matatizo ya kinga ya mwili.
Homa ya ini A (Hepatitis A virus)
Husababishwa na virusi vya homa ya ini A, yani Hepatitis A (HAV)
Huambukizwa kwa kula chakula au kunywa maji machafu
Mara nyingi hupona bila kuhitaji matibabu makubwa inaweza ikawa na matibabu ya muda mfupi au mfumo wa lishe pekee
Mara nyingi sana Hepatitis A huwa ni ya muda mfupi na gaibadiliki kuwa sugu hupona yenyewe bila dawa.
Homa ya ini B (Hepatitis B virus)
Husababishwa na virusi vya homa ya ini B yani Hepatitis B (HBV)
Huambukizwa kupitia damu, ngono, au mama kwenda kwa mtoto katika kipindi cha ujauzito au kujifungua
Inaweza kuwa ya muda mfupi (acute isiyo hitaji matibabu ) au ya muda mrefu (sugu yenye kuhitaji matibabu ya kina matibabu ya muda mlefu hadi tatizo kuisha au kupona kwa mgonjwa)
Sugu inaweza kusababisha saratani ya ini, kovu sugu la ini yani (cirrhosis) na ini kuferi
Homa ya ini C ( Virus vya hepatitis C)
Husababishwa na virusi vya homa ya ini C yani Hepatitis C (HCV)
Mara nyingi huambukizwa kwa damu (hasa sindano na ngono)
Ina uwezekano mkubwa wa kuwa sugu na matibabu yake huchukua muda mlefu kupona moja kwa moja
Huongeza hatari ya ini kushindwa kufanya kazi au kupata saratani na kupelekea ini kusinyaa au kuferi kabisa
Homa ya ini D (Hepatitis D virus)
Hutokea kwa watu wenye kuishi na maambukizo ya hepatitis B pekee
Husababisha maambukizi makali zaidi ya ini
Homa ya ini E (Hepatitis E virus)
Huambukizwa kwa njia ya chakula au maji machafu
Hepatitis E kwa baadhi ya wagonjwa hupona yenyewe kwa kawaida bila dawa
Homa ya ini inaweza kuwa hatari kwa wajawazito
BAADHI YA DALILI ZA HOMA YA INI YA MUDA MLEFU ISIYO TIBIWA
Miwasho sugu ya ngozi
Uchovu wa mara kwa mara na mkali
Maumivu upande wa kulia juu ya tumbo
Macho au ngozi kuwa ya njano (jaundice)
Kichefuchefu cha mara kwa mara na muda mwengine kutapika
Homa za mara kwa mara zisizo isha
Mgonjwa anapitia hali ya kupoteza hamu ya kula
Mgonjwa hupata mkojo wenye rangi ya njano sana, na kinyesi kuwa cha rangi ya udongo
VIPIMO NA MATIBABU YA HOMA YA INI (HEPATITIS)
Vipimo vya damu hutumika kugundua aina ya virusi (HBsAg Hepatitis B surface antigen au Antigen)
Vipimo vya ini vya Liver Function Tests (LFTs) kuangalia kazi ya ini
Ultrasound au biopsy inaweza kufanyika kwa hali sugu
Matibabu hutegemea na aina ya hepatitis, baadhi hupona yenyewe bila dawa, nyingine huhitaji dawa za muda mrefu katika kutibu.
Ikiwa unahitaji matibabu zaidi ya homa ya ini pamoja na maelezo zaidi kuhusu aina fulani kama Hepatitis B au C, au kuhusu chanjo na kinga, niambie nikusaidie zaidi.
KIPIMO HIKI, HUASHIRIA MTU AMEAMBUKIZWA VIRUS VYA HOMA YA INI B (KIPIMO KINAONYESHA MISTARI MIWILI)
Kwa mtu alie ambukizwa virus vyab hepatitis B na kama hajafikia matibabu na kupona basi kipimo cha hepatitis b surfece antigen kitaonyesha mistari kuashia Positive.
NEGATIVE (KIPIMO HIKI KINAONYESHA MSTARI MMOJA KUASHIRIA NEGATIVE, HANA MAAMBUKIZI YA HBV)
Mtu amepona kutoka katika mambukizi ya hepatitis B baada ya matibabu ya muda fulani katika maisha maisha yake
BAADHI YA MADHARA HATARISHI YA HOMA YA INI YA MUDA MLEFU ISIYO TIBIWA (CHRONIC HEPATITIS)
Tumbo kuvimba kwakujaa maji (Asciets), miguu kuvimba (Edema) pamoja na kupumua kwa shida
Kupungukiwa damu (mgonjwa kupungukiwa damu kwasababu ya kutapika damu na upungufu wa virutubisho mwilini), kuharibika kwa seli nyekundu za damu.
Ini kuvimba na kupata kovu sugu, ambalo husababisha cirrhosis ya ini
Mgonjwa kupata saratani ya kudumu ya ini na kusababisha ini kusinyaa na kushindwa kufanya kazi zake vizuri (liver failure)
Kupungua uzito, kukonda, kukosa hamu ya kula na kupoteza nguvu hasa mifupa
- Kupata vidonda sugu vya tumbo na saratani ya utumbo mpana
KUMBUKA:- Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.
Karibu tukuhudumie, kwa changamoto za afya, tunatoa huduma za VIPIMO, MATIBABU, USHAURI na CHANJO