𝗔𝗳𝘆𝗮𝘆𝗮𝗻𝗴𝘂 𝗖𝗼𝗺𝗽𝗮𝗻𝘆 𝗟𝘁𝗱
Ni taasisi ya Afya, iliyosajiliwa nchini Tanzania kwakuidhinishwa kutoa huduma zake za kiafya, Matibabu, chanjo pamoja na vifaa tiba kama vile Dawa ambavyo kwa pamoja vimethibitishwa na ya taasisi kuu zinazohusika na kuthibitisha usalama wa dawa na vifaa tiba nchini Tanzania:
𝟭. 𝗠𝗮𝗺𝗹𝗮𝗸𝗮 𝘆𝗮 𝗗𝗮𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗩𝗶𝗳𝗮𝗮 𝗧𝗶𝗯𝗮 (𝗧𝗠𝗗𝗔)
Hii ndiyo taasisi kuu ya serikali inayosimamia usajili, ubora, usalama na ufanisi wa dawa, chanjo, vitendanishi na vifaa tiba kabla havijatumika kwa wananchi.
TMDA huangalia majaribio ya kitaalamu (clinical na laboratory data) na kuhakikisha bidhaa zimekidhi viwango vya kimataifa.
𝟮. 𝗕𝗮𝗿𝗮𝘇𝗮 𝗹𝗮 𝗙𝗮𝗺𝗮𝘀𝗶 𝗹𝗮 𝗧𝗮𝗻𝗴𝗮𝗻𝘆𝗶𝗸𝗮 (𝗣𝗖𝗧 – 𝗣𝗵𝗮𝗿𝗺𝗮𝗰𝘆 𝗖𝗼𝘂𝗻𝗰𝗶𝗹 𝗼𝗳 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮)
Linasimamia usajili na utoaji leseni kwa wataalamu wa famasia. Huhakikisha utunzaji sahihi, usambazaji na matumizi bora ya dawa nchini.
𝟯. 𝗪𝗶𝘇𝗮𝗿𝗮 𝘆𝗮 𝗔𝗳𝘆𝗮 – 𝗜𝗱𝗮𝗿𝗮 𝘆𝗮 𝗞𝗶𝗻𝗴𝗮 𝗻𝗮 𝗜𝗱𝗮𝗿𝗮 𝘆𝗮 𝗧𝗶𝗯𝗮
Kwa kushirikiana na TMDA, hufuatilia utekelezaji wa sera na miongozo ya kitaifa kuhusu dawa na vifaa tiba. Pia hutoa miongozo ya kitaifa ya matumizi sahihi.
𝟰. 𝗕𝗮𝗿𝗮𝘇𝗮 𝗹𝗮 𝗠𝗮𝗱𝗮𝗸𝘁𝗮𝗿𝗶 𝗧𝗮𝗻𝗴𝗮𝗻𝘆𝗶𝗸𝗮 (𝗠𝗲𝗱𝗶𝗰𝗮𝗹 𝗖𝗼𝘂𝗻𝗰𝗶𝗹 𝗼𝗳 𝗧𝗮𝗻𝗴𝗮𝗻𝘆𝗶𝗸𝗮 – 𝗠𝗖𝗧)
Linahakikisha madaktari wanaotoa dawa wanazingatia miongozo ya kitaalamu. Hupitia malalamiko au madhara yatokanayo na matumizi ya dawa.
𝟱. 𝗧𝗮𝗮𝘀𝗶𝘀 𝘇𝗮 𝗨𝘁𝗮𝗳𝗶𝘁𝗶 𝗡𝗜𝗠𝗥 (𝗡𝗮𝘁𝗶𝗼𝗻𝗮𝗹 𝗜𝗻𝘀𝘁𝗶𝘁𝘂𝘁𝗲 𝗳𝗼𝗿 𝗠𝗲𝗱𝗶𝗰𝗮𝗹 𝗥𝗲𝘀𝗲𝗮𝗿𝗰𝗵)
Hufanya tafiti za kiafya, ikiwa ni pamoja na majaribio ya kitaalamu ya dawa na chanjo kabla ya kupitishwa na 𝗧𝗠𝗗𝗔.
𝗧𝗠𝗗𝗔 Ndiyo mhimili mkuu wa kuthibitisha usalama wa dawa na vifaa tiba Tanzania, kisha taasisi nyingine husaidia katika usimamizi, utafiti, na matumizi yake kwa wananchi.
Afya Yangu ni taasisi ambayo ilianza kufanya kazi kikamilifu mnamo Agosti 2019 ikiwa na Makao Makuu yake Dar es Salaam Tanzania Afrika Mashariki.
Kama viumbe vilivyo hai, pia kampuni inakadiriwa kukua na kufungua matawi mengine ndani na nje ya nchi ya Tanzania 🇹🇿 kwaajili ya kusogeza huduma kwa ukaribu zaidi katika jamii.
Kampuni huchota mawazo chanya na mitazamo tofauti tofauti kuanzia mwanzo kwakuzingatia shauku ya Mwanzilishi ambaye ni mtaalamu wa matibabu aliye na uzoefu wa hali ya juu wa ndani na kimataifa akifanya kazi katika vituo vya afya vya umma na vya kibinafsi.
Sekta ya huduma ya afya imebadilika kwa muda na ushahidi wa mabadiliko katika muundo wa magonjwa na suluhisho zinazotolewa. Ingawa magonjwa ya kuambukiza kama 𝗛.𝗜.𝗩, 𝗛𝗘𝗣𝗔𝗧𝗜𝗧𝗜𝗦 𝗡𝗔 𝗦𝗬𝗣𝗛𝗜𝗟𝗜𝗦, yaligharimu maisha ya watu wengi katika karne ya 19 hadi sasa.
Kumekuwa na mabadiliko ya mwelekeo wa magonjwa yasiyoambukiza na ulemavu wa kudumu ambayo huitaji suluhisho jipya kama ukombozi katika nyanja ya Afya ni mtazamo mpya wa kitabibu tofauti na matibabu yale ya awali.
Enzi ya utambuzi wa kimwili, uchunguzi, kuzuia na matibabu ya magonjwa mbalimbali inabadilishwa na ufumbuzi wa kidigital na hivi karibuni umeendelezwa kwa akili ya bandia kama njia ya kisasa ya kukabiliana na changamoto zinazohusiana na afya.
𝗔𝗳𝘆𝗮𝘆𝗮𝗻𝗴𝘂 𝗖𝗼𝗺𝗽𝗮𝗻𝘆 𝗟𝘁𝗱 inajitolea kuwa kitovu cha suluhisho bora kwa changamoto mbalimbali zinazohusiana na afya zinazoathiri jamii, mifumo ya afya na sekta kwa ujumla.
Kupitia mbinu za kibunifu tunajionyesha kama 𝗧𝗵𝗶𝗻𝗸 𝘁𝗮𝗻𝗸 ili kutoa Suluhisho yaliyojaribiwa ndani lakini bado yamethibitishwa kisayansi kwa changamoto zetu za sasa na zijazo zinazohusiana na afya.
Tunaamini katika kupata Suluhu kwa kila changamoto na ujasiri wetu unatokana na nguzo zetu kuu tano: