Vitamini B-12 ni vitamini ambayo mwili hutumia kutengeneza na kusaidia seli za ini pamoja na seli za neva iweze kuwa na afya zaidi. Pia hutumika kutengeneza seli nyekundu za damu zenye afya na nyenzo za kijeni ndani ya seli zinazoitwa DNA. Vitamini B-12 pia inaitwa cobalamin. Vyanzo vya chakula vya vitamini B-12 ni pamoja na kuku, samaki na bidhaa za maziwa.
Ugonjwa wa figo kuwa na mawe umeenea sana.Husababisha maumivu makali sana.Wakati mwingine mawe ya figo hayaonyeshi dalili zozote.Ugonjwa huu husababisha maambukizi na kupata hudhuru wa figo kwa wagonjwa wengine,iwapo hautotibiwa haraka.Mawe yatokeapo huwa ni rahisi kurudia tena kwa hiyo ni muhimu kuelewa , jinsi ya kuzuia na kukabiliana na ugonjwa huu.
Vidonda vya tumbo (kwa Kiingereza: "gastritis") ni miongoni mwa magonjwa ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula katika mwili wa binadamu. Huo ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi sana duniani na huwapata sanasana watu wazima kuliko watoto wadogo.