Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Figo kuwa na mawe - Ni ugonjwa unao sababisha figo kuwa na mawe


Ugonjwa wa figo kuwa na mawe umeenea sana.Husababisha maumivu makali sana.Wakati mwingine mawe ya figo hayaonyeshi dalili zozote.Ugonjwa huu husababisha maambukizi na kupata hudhuru wa figo kwa wagonjwa wengine,iwapo hautotibiwa haraka.Mawe yatokeapo huwa ni rahisi kurudia tena kwa hiyo ni muhimu kuelewa , jinsi ya kuzuia na kukabiliana na ugonjwa huu.

𝗙𝗜𝗚𝗢 𝗞𝗨𝗪𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗪𝗘 - 𝗩𝗜𝗦𝗔𝗕𝗔𝗕𝗜𝗦𝗛𝗜 VYA UGONJWA WA FIGO KUWA NA MAWE, 𝗗𝗔𝗟𝗜𝗟𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗔𝗪𝗔𝗟𝗜:


Figo kuwa na mawe ni hali inayojulikana kitaalamu kama “𝗸𝗶𝗱𝗻𝗲𝘆 𝘀𝘁𝗼𝗻𝗲𝘀” au 𝗡𝗲𝗽𝗵𝗿𝗼𝗹𝗶𝘁𝗵𝗶𝗮𝘀𝗶𝘀. Ni hali ambapo madini na chumvi zilizomo kwenye mkojo hukusanyika na kuunda mawe madogo au makubwa ndani ya figo.


✔️ 𝗕𝗮𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗦𝗮𝗯𝗮𝗯𝘂 𝗸𝘂𝘂 𝘇𝗮 𝗳𝗶𝗴𝗼 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘄𝗲:

 

  • Kunywa maji kidogo – mkojo kuwa mzito na kurahisisha mawe kuunda.

     

  • Kiasi kikubwa cha madini kama calcium, oxalate au uric acid kwenye mkojo.

     

  • Lishe yenye chumvi na protini nyingi.

     

  • Magonjwa ya mfumo wa mkojo au tezi za homoni.

     

  • Historia ya kifamilia – kurithi tabia ya kupata mawe.


✔️ 𝗕𝗮𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗗𝗮𝗹𝗶𝗹𝗶 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘇𝗼𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗼𝗻𝗲𝗸𝗮𝗻𝗮:

 

  • Maumivu makali ya ghafla upande wa mgongo au kiunoni (colic).

     

  • Mkojo wenye damu.

     

  • Maumivu yanayosambaa hadi tumboni au kwenye nyonga.

     

  • Kukojoa mara kwa mara au kwa shida.

     

  • Kichefuchefu na kutapika.


✔️ 𝗠𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮𝗯𝘂 𝘆𝗮 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗳𝗶𝗴𝗼:

 

  • Kunywa maji mengi (angalau lita 2–3 kwa siku).

     

  • Dawa za kuondoa na kuzuia maumivu na kusaidia mawe madogo kutoka yenyewe.

     

  • Matibabu ya kuvunja mawe kwa mawimbi ya mshtuko (lithotripsy).

     

  • Upasuaji mdogo endapo mawe ni makubwa au yameziba njia ya mkojo.


𝗡𝗢𝗧𝗘: Kwa mtu mwenye mawe ya figo, inashauriwa kupimwa ili kubaini ukubwa na aina ya mawe na kupata matibabu sahihi.

 



𝗠𝗨𝗛𝗧𝗔𝗦𝗔𝗥𝗜 𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘 𝗞𝗨𝗢𝗡𝗬𝗘𝗦𝗛𝗔 𝗡𝗔𝗠𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗪𝗘 𝗬𝗔𝗡𝗔𝗩𝗬𝗢𝗡𝗨𝗡𝗗𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘 𝗙𝗜𝗚𝗢:

Huu hapa ni muhtasari rahisi wa mchakato jinsi mawe yanavyotokea kwenye figo hatua kwa hatua:


🔹 Hatua kwa Hatua za Uundwaji wa Mawe ya Figo


✔️ 𝗨𝗽𝘂𝗻𝗴𝘂𝗳𝘂 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗷𝗶 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶𝗻𝗶 𝘆𝗮𝗻𝗶 𝗠𝗮𝗷𝗶 𝗸𝗶𝗱𝗼𝗴𝗼 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶𝗻𝗶

 

Mtu anapokunywa maji machache → mkojo unakuwa mkali (concentrated).


✔️ 𝗠𝗮𝗱𝗶𝗻𝗶 𝗻𝗮 𝗰𝗵𝘂𝗺𝘃𝗶 𝗸𝘂𝘇𝗶𝗱𝗶 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗸𝗼𝗷𝗼

 

Calcium, oxalate, au uric acid zinapozidi → zinakosa kutengenezwa vizuri.

 

✔️ 𝗞𝘂𝘄𝗲𝗽𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗲𝗺𝗯𝗲𝗰𝗵𝗲𝗺𝗯𝗲 𝗻𝗱𝗼𝗴𝗼 (𝗰𝗿𝘆𝘀𝘁𝗮𝗹𝘀)

 

Madini chumvi na urea huanza kuganda na kuunda fuwele ndogo.


𝗙𝘂𝘄𝗲𝗹𝗲 𝗸𝘂𝘀𝗵𝗶𝗸𝗮𝗺𝗮𝗻𝗮 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 𝗻𝗱𝗮𝗻𝗶 𝘆𝗮 𝗳𝗶𝗴𝗼

 

Fuwele zinapoungana → zinaunda “jiwe” dogo la mwanzo.

 

✔️ 𝗝𝗶𝘄𝗲 𝗸𝘂𝗸𝘂𝗮 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 𝗻𝗮 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 𝗸𝘄𝗮𝗸𝗮𝗱𝗶𝗿𝗶 𝘀𝗶𝗸𝘂 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘃𝘆𝗼 𝘇𝗶𝗱𝗶 𝗸𝘄𝗲𝗻𝗱𝗮 𝗻𝗮 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗸𝘂𝘁𝗶𝗯𝗶𝘄𝗮

 

Kadri mkojo unavyoendelea kubeba madini mengi → jiwe hukua taratibu.


✔️ 𝗞𝘂𝘇𝗶𝗯𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗻𝗷𝗶𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗸𝗼𝗷𝗼

 

Jiwe likiwa kubwa → linaweza kushuka kutoka figo kwenda ureta (bomba la mkojo) na kuziba njia → kusababisha maumivu makali.


𝗞𝘄𝗮 𝘂𝗳𝘂𝗽𝗶:

Maji kidogo + Madini kuzidi + Fuwele kushikamana = Jiwe la figo

 

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨, 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗝𝗢 𝗡𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜:

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!