ALT (Alanine Aminotransferase) na AST (Aspartate Aminotransferase)
Kipimo chakutambua Enzymes ya ini kama (ALT na AST), ni kipimo muhimu sana kwa
UNAFAHAMU NINI KUHUSU KUZIDI KWA ENZYMES (VIMENG'ENYA) ALT NA AST KATIKA VIPIMO VYAKO:
ALT (Alanine Aminotransferase) na AST (Aspartate Aminotransferase) ni enzymes zinazopatikana kwa wingi kwenye seli za ini (na sehemu ndogo kwenye misuli, moyo na figo).
Kiwango cha juu cha ALT na AST kwenye damu kina maana kwamba seli za ini (hepatocytes) zimeumia au kuharibiwa na hivyo kuruhusu enzymes hizi kutoka kwenye seli kuingia kwenye damu.
Hii si ugonjwa peke yake, bali ni ishara kwamba kuna tatizo au shinikizo kwenye ini au viungo vinavyohusiana.
BAADHI YA SABABU ZINAZO WEZA KUONGEZA ALT NA AST
1. Homa ya ini (Hepatitis A, B, C, E) – Maambukizi ya virusi huumiza seli za ini.
2. Matumizi ya pombe – Pombe huunguza na kuharibu tishu za ini.
3. Mafuta mengi kwenye ini (Fatty liver) – Inaweza kutokana na unene, kisukari au matumizi ya pombe.
4. Dawa zenye sumu kwa ini – Mfano: Paracetamol kupita kiasi, dawa za TB, antibiotics fulani, dawa za saratani.
5. Saratani ya ini au uvimbe – Huharibu seli na kusababisha enzymes kuongezeka.
6. Kuziba kwa njia ya nyongo (Bile duct obstruction) – Mawe kwenye nyongo au uvimbe husababisha shinikizo kwenye ini.
7. Magonjwa ya kinga mwili dhidi ya ini (Autoimmune hepatitis) – Kinga mwili hushambulia ini.
8. Msongo mkubwa wa ini (Ischemic hepatitis) – Matokeo ya shinikizo la damu kushuka sana au mshtuko wa moyo.
9. Maambukizi mengine – Kama malaria kali, leptospirosis, au maambukizi ya bakteria yanayofika kwenye ini.
10. Uharibifu wa misuli (muscle injury) – Hasa AST, inaweza kupanda pia kutokana na ajali au mazoezi mazito kupita kiasi.
KUMBUKA:
ALT kwa kawaida inaonyesha zaidi matatizo ya ini,
AST inaweza kuongezeka pia kwenye matatizo ya moyo au misuli.
Kiwango cha juu kinaweza kuhitaji vipimo vya ziada kama Bilirubin, ALP, GGT, na Ultrasound ili kubaini chanzo.
Karibu kwa huduma ya vipimo, ushauri, matibabu na chanjo ya homa ya ini B.
Kwa huduma zaidi ya vipimo, chanjo na matibabu, unaweza kufika hapa kituoni kwakuweka appointiment kupitia website kwakujaza fomu inayo tokea mbele yako, kupiga simu au kutuna ujumbe mfupi wa maandishi kupitia WhatsApp +255628361104: