Hatua za ugonjwa wa ini na saratani ya ini - Tambua dalili za awali na matibabu
Hatua kuu nne za ugonjwa wa ini na saratani - hatua ambazo baadhi ya wagonjwa wanaweza kupitia dalili mbali mbali nyepesi nyepesi na hatarishi
Hatua za ugonjwa wa ini na saratani (hepatocellar carsnoma)
Homa ya ini ni uvimbe wa ini unao husishwa na seli za ini kuvimba zaidi katika tishu za ini.
Hali hii inaweza kujiponyesha yenyewe bila kuhitaji matibabu, lakini inaweza kuhitaji matibabu ya haraka kama itaendelea kudumu kwa muda mlefu kama vile miezi sita hadi mwaka, na pindi hatua za matibabu zisipo chukuliwa uvimbe huu unaweza kuendelea kuwa fibrosisi, cirrhosis na saratani ya ini.
Kuvimba kwa ini au homa ya ini, inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali pindi tu tahadhari isipo zingatiwa.
1. Homa ya ini inaweza kusababishwa na mtindo mbovu wa maisha kama vile ulaji wa vyakula vyenye kupikwa na mafuta mengi, chumvi nyingi au sukari.
2. Homa ya ini pia inaweza kusababishwa na maambukizi ya virus kama vile hepatitis A, Hepatitis B, Hepatitis C, Hepatitis D au hepatitis E. Maambukizi haya yanaweza kudumu kwa miaka mingi bila mgonjwa kuona dalili yoyote, baadhi ya wagonjwa huona dalili ndani ya miezi michache tu baada ya kuambukizwa, lakini baadhi ya wagonjwa wanaweza kuishi miaka mingi pasipo kuona dalili yoyote, dalili huja kuonekana baada ya miaka kadhaaa.
3. Lakini pia homa ya ini, inaweza kusababishwa na maambukizi ya minyoo wa kichocho (Schistosoma), minyoo hii inapo dumu kwa muda mlefu, huendelea kuzaliana kwakutaga mayai yao kwenye mishipa ya potal ya ini, kutaga kwao mayai huchochea ini kuvimba na kusababisha saratani ya ini.
4. Homa ya ini pia inaweza kusababishwa na matatizo ya kinga ya mwili (autoimmune hepatitis) mwili unapo zalisha kinga kupita kiasi pasipo udhibiti, huchochea mkusanyiko wa seli zisizo na kazi kwenye tishu za ini, na kupelekea ini kuvimba.
𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗛𝗨𝗣𝗜𝗧𝗜𝗔 𝗛𝗔𝗧𝗨𝗔 𝗞𝗨𝗨 𝗡𝗡𝗘 (𝟰) 𝗛𝗔𝗗𝗜 𝗜𝗡𝗜 𝗞𝗨𝗙𝗘𝗥𝗜 𝗔𝗨 𝗞𝗨𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗙𝗔𝗡𝗬𝗔 𝗞𝗔𝗭𝗜.
Hatua za saratani ya ini, Ni mchakato mgumu, lakini kwa njia iliyorahisishwa zaidi, inajumuisha hatua kuu nne za saratani ya ini:
1. Hatua ya 1: Uvimbe kwenye ini.
2. Hatua ya 2: Uvimbe mmoja au zaidi hupatikana kwenye ini au umeenea kwenye mishipa ya damu iliyo karibu na ini.
3. Hatua ya 3: Katika hatua hii, zaidi ya tumor yani vimbe kubwa moja ipo katika ini. Uvimbe mmoja unaweza kuwa takribani sentimeta 5cm. Hapa, saratani pia imeenea kwa mishipa mikubwa ya damu, viungo vingine, au nodi za lymph.
4. Hatua ya 4: Saratani imeenea katika sehemu nyingine za mwili kama viungo vingine au nodi za limfu.
Katika hatua izo za saratani ya ini kunaweza kuwa na matukio zaidi yanayoweza kutokea, kama vile dalili za awali na dalili za kudumu zinazo ashilia hatua za mwisho za ugonjwa mkali wa ini.
Kwa maelezo zaidi kuhusu homa ya ini, vipimo na matibabu kufika kituoni kwakuweka appointiment kwenye tovuti kwakujaza fomu au kupiga simu moja kwa moja kupitia huduma kwa wateja: +255746484873