Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Makundi 10 ya waathirika wa homa ya ini wenye nafasi ndogo sana ya kupona kabisa,


Makundi 10 ya waathirika wa homa ya ini wenye nafasi ndogo sana ya kupona kabisa, hasa ikiwa hawapati matibabu kwa wakati au hawafuati ushauri wa kiafya.

𝗠𝗔𝗞𝗨𝗡𝗗𝗜 (𝟭𝟬) 𝗬𝗔 𝗪𝗔𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗜𝗡𝗜 𝗪𝗔𝗟𝗜𝗢 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗡𝗔𝗙𝗔𝗦𝗜 𝗡𝗗𝗢𝗚𝗢 𝗦𝗔𝗡𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗣𝗢𝗡𝗔 𝗞𝗔𝗕𝗜𝗦𝗔:


Hii inaweza kusababisha ugonjwa kuwa sugu zaidi, ini kusinyaa, kuharibu ini au hata kusababisha saratani ya ini na hata kifo:


𝗪𝗮𝗻𝗮𝗼𝗴𝘂𝗻𝗱𝘂𝗹𝗶𝘄𝗮 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘇𝗮 𝗺𝘄𝗶𝘀𝗵𝗼 (𝗮𝗱𝘃𝗮𝗻𝗰𝗲𝗱 𝗹𝗶𝘃𝗲𝗿 𝗱𝗶𝘀𝗲𝗮𝘀𝗲)

Wagonjwa wanaogunduliwa wakati tayari wana 𝗰𝗶𝗿𝗿𝗵𝗼𝘀𝗶𝘀 au kansa ya ini (𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗼𝗰𝗲𝗹𝗹𝘂𝗹𝗮𝗿 𝗰𝗮𝗿𝗰𝗶𝗻𝗼𝗺𝗮) nafasi yao ya kupona ni ndogo sana.


 


𝗪𝗮𝗹𝗲 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗼𝗽𝘂𝘂𝘇𝗶𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮𝗯𝘂 𝗮𝘂 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗳𝘂𝗮𝘁𝗮 𝗺𝗮𝗮𝗴𝗶𝘇𝗼 𝗻𝗮 𝘂𝘀𝗵𝗮𝘂𝗿𝗶 𝘄𝗮 𝗸𝗶𝘁𝗮𝗯𝗶𝗯𝘂 𝗻𝗮 𝗺𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺𝘂 𝘄𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮

Kupuuza dalili unazo ziona, Kutokumaliza dawa au dozi, kupuuza ratiba za vipimo, au kujitibu kienyeji kama mitishamba, huchelewesha kupona au kuzidisha hali kuwa mbaya zaidi.

 

𝗪𝗮𝗮𝘁𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗮 𝘄𝗮 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗕 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗼𝗽𝗮𝘁𝗮 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗸𝗶𝘄𝗮 𝘄𝗮𝘁𝗼𝘁𝗼 𝘄𝗮𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮

Watoto wachanga waliopata maambukizi kutoka kwa mama (mother-to-child transmission) huwa katika hatari kubwa ya ugonjwa wa ini kuwa sugu zaidi na kusababisha kansa ya ini na ini kusinyaa.

 

𝗪𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗛𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗖 𝗮𝗺𝗯𝗮𝗼 𝗵𝗮𝘄𝗮𝗽𝗮𝘁𝗶 𝗺𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮𝗯𝘂 𝗺𝗮𝗽𝘆𝗮 (𝗗𝗔𝗔𝘀)

Wale wanaoendelea kutumia dawa za zamani kama vile Truvada na Tenofovir au kutopata tiba kabisa huwa na uwezekano mdogo wa kupona.

 

𝗪𝗮𝗹𝗲 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗼𝗲𝗻𝗱𝗲𝗹𝗲𝗮 𝗸𝘂𝘁𝘂𝗺𝗶𝗮 𝗽𝗼𝗺𝗯𝗲 𝗮𝘂 𝗱𝗮𝘄𝗮 𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗹𝗲𝘃𝘆𝗮

Pombe huongeza kasi ya uharibifu wa ini. Matumizi haya huathiri sana tiba na huongeza hatari ya kushindwa kupona kabisa.

 


𝗪𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝗺𝗲𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝘀𝘂𝗴𝘂 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝗛𝗜𝗩, 𝗸𝗶𝘀𝘂𝗸𝗮𝗿𝗶, 𝗮𝘂 𝘀𝗵𝗶𝗻𝗶𝗸𝗶𝘇𝗼 𝗹𝗮 𝗱𝗮𝗺𝘂

Magonjwa haya huathiri kinga ya mwili na hufanya ini kushindwa kujitibu ipasavyo na kuweka upinzani kwenye dawa na kinga ya mwili.

 

𝗪𝗮𝗻𝗮𝗼𝘁𝘂𝗺𝗶𝗮 𝗱𝗮𝘄𝗮 𝘇𝗮 𝘀𝘂𝗺𝘂 𝗸𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗯𝗶𝗹𝗮 𝘂𝘀𝗵𝗮𝘂𝗿𝗶 𝘄𝗮 𝗱𝗮𝗸𝘁𝗮𝗿𝗶 (𝗺𝗳𝗮𝗻𝗼 𝗯𝗮𝗮𝗱𝗵𝗶 𝘆𝗮 𝗱𝗮𝘄𝗮 𝘇𝗮 𝗺𝗶𝘁𝗶𝘀𝗵𝗮𝗺𝗯𝗮)

Dawa zisizo salama au za kienyeji zinazochosha ini huchangia kuharibu ini zaidi.

 


𝗪𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗼𝗸𝗼 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗮𝘇𝗶𝗻𝗴𝗶𝗿𝗮 𝘆𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝘀𝗼𝗻𝗴𝗼 𝗺𝗸𝘂𝗯𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝘄𝗮𝘇𝗼 𝗮𝘂 𝗹𝗶𝘀𝗵𝗲 𝗱𝘂𝗻𝗶

Mwili usio na lishe bora au unaoshambuliwa na stress huwa dhaifu katika kupambana na virusi.

 

𝗪𝗮𝘁𝘂 𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗵𝗶𝘀𝘁𝗼𝗿𝗶𝗮 𝘆𝗮 𝗳𝗮𝗺𝗶𝗹𝗶𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝗮𝗻𝘀𝗮 𝘆𝗮 𝗶𝗻𝗶 𝗮𝘂 𝘂𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶

Hii huongeza hatari ya ugonjwa kutokuwa na mwisho mzuri kwa sababu ya urithi wa kinasaba (genetic risk).

 

𝗪𝗮𝗮𝘁𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗮 𝘄𝗮 𝗵𝗲𝗽𝗮𝘁𝗶𝘁𝗶𝘀 𝗕 𝗮𝘂 𝗖 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗼𝗸𝗼 𝘃𝗶𝗷𝗶𝗷𝗶𝗻𝗶 𝗯𝗶𝗹𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘇𝗮 𝗸𝗶𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮𝗺𝘂

Kukosa vipimo sahihi, ushauri wa kitaalamu, na dawa za kisasa hupunguza sana nafasi ya kupona.


 


𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!