Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Ugonjwa wa bawasiri, chanzo, dalili, vipimo na matibabu


Suluhisho la ugonjwa wa bawasiri - Bawasiri (kwa Kiingereza Hemorrhoids) ni uvimbe au kujaa kwa mishipa ya damu kwenye sehemu ya haja kubwa (rectum) au nje ya tundu la haja kubwa (anus).

 

UGONJWA WA BAWASIRI, VISABABISHI, DALILI, MADHARA NA MATIBABU

Mishipa ya eneo la tundu la haja kubwa, Mishipa hii inapovimba au kujeruhiwa, husababisha maumivu, kuwasha, na wakati mwingine kutokwa na damu.

Aina kuu za bawasiri


1. Bawasiri za ndani (Internal hemorrhoids)

 

  • Zipo ndani ya haja kubwa.

     

  • Mara nyingi haziumi, lakini zinaweza kusababisha damu kwenye choo.

 

2. Bawasiri za nje (External hemorrhoids)

 

  • Zipo nje ya tundu la haja kubwa.

 

  • Huweza kuuma sana, kuwasha, na kuvimba.

 

3. Bawasiri zilizo na damu iliyoganda (Thrombosed hemorrhoids)

 

  • Ni bawasiri za nje ambazo mishipa yake imeganda damu.

     

  • Husababisha maumivu makali na uvimbe mkubwa.

 



Sababu za kusababisha bawasiri

 

  • Vidonda vya tumbo vya muda mlefu

     

  • Kukaa au kusimama kwa muda mrefu.

     

  • Kufanya choo kigumu (constipation) au kuharisha mara kwa mara.

     

  • Kushinikiza sana wakati wa kujisaidia.

     

  • Uzito mkubwa au ujauzito (shinikizo kwenye mishipa ya sehemu ya haja kubwa).

     

  • Kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber).

     

  • Umri mkubwa (mishipa inakosa uimara).

 

Dalili za bawasiri

 

  • Choo kigumu na muda mwingine kukosa choo kabisa kwa muda mlefu

     

  • Kutokwa na damu nyekundu wakati wa kujisaidia.

     

  • Kuwasha au kuchoma sehemu ya haja kubwa.

     

  • Uvimbe au kinyama sehemu ya tundu la haja kubwa.

     

  • Maumivu wakati wa kujisaidia au kukaa.

 

Matibabu

 

1. Mabadiliko ya mtindo wa maisha

 

  • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi (mboga, matunda, nafaka zisizokobolewa).

     

  • Kunywa maji ya kutosha kila siku.

     

  • Epuka kukaa muda mrefu kwenye choo.

     

  • Fanya mazoezi mara kwa mara.

 

2. Matibabu ya kitabibu

 

  • Matibabu ya dawa salama za kuzuia na kuondoa uvimbe wa kinyama cha bawasiri

     

  • Dawa za kuimarisha mfumo wa chakula, kama vile kulainisha choo, mmeng'enyo

     

  • Dawa za kuzuia na kuondoa gesi tumboni

     

  • Kufunga mishipa kwa mpira mdogo (rubber band ligation).

     

  • Matibabu kwa laser au sindano maalum.

     

  • Upasuaji (kama bawasiri imezidi sana au imejirudia mara kwa mara).

     

Kama bawasiri haitatibiwa mapema, inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya kiafya na usumbufu wa kudumu. Madhara yake ni pamoja na:

 

1. Kutokwa na damu kwa muda mrefu

 

Bawasiri inaweza kusababisha damu kutoka kila mara unapojisaidia.

Hii huongeza hatari ya upungufu wa damu (anemia), hali inayosababisha udhaifu, kizunguzungu, na kupungukiwa pumzi.


2. Maambukizi

 

Vidonda vilivyo wazi kwenye bawasiri vinaweza kuambukizwa na bakteria, na kusababisha uvimbe mkubwa, usaha, na homa.


3. Maumivu makali na uvimbe

 

Bawasiri kubwa au iliyoganda damu (thrombosed hemorrhoid) husababisha maumivu yasiyovumilika, hasa unapokaa au kutembea.

 

4. Shida ya kujisaidia

 

Woga wa maumivu wakati wa choo unaweza kumfanya mgonjwa ashikilie choo, hali inayoongeza constipation na kufanya bawasiri izidi kuwa mbaya.

 

5. Kupoteza udhibiti wa haja ndogo au kubwa


Endapo mishipa na misuli ya eneo la haja kubwa itaathirika sana, inaweza kusababisha kudhoofika kwa misuli ya kufunga haja, na mtu kuvuja haja bila kutarajia.

 

6. Kuongezeka ukubwa na kujaa nje (Prolapse)

 

Bawasiri inaweza kushuka na kubaki nje ya tundu la haja kubwa, na mara nyingine haiwezi kurudi ndani bila msaada wa kitabibu.

 

7. Hatari ya ugonjwa mwingine kufichwa

 

Hatari za bawasiri, 

  • kama kutokwa damu kwenye choo, zinaweza kufanana na dalili za saratani ya utumbo mpana. Kutotibiwa kunaweza kuchelewesha kugundua ugonjwa mkubwa zaidi.


Kumbuka:


Bawasiri inaweza kupona kabisa kwa hatua rahisi kama ikitibiwa mapema, lakini ukiona damu nyingi, maumivu makali, au uvimbe mkubwa—ni muhimu kumuona daktari mara moja kwaajili ya vipimo vikubwa.

 

Tunaweza kukupa orodha ya vyakula bora vya kuku saidia au kumsaidia mgonjwa wa bawasiri na vile anavyopaswa kuepuka ili kupona haraka akiwa katika matibabu.


Unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kwakupiga simu au kutuna ujumbe mfupi wa maandishi kupitia +255628361104  +255746484873


𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!