Fatty liver (Ugonjwa wa ini wa mafuta)
Ugonjwa wa ini wa mafuta (Fatty liver diseases) unasababishwa na mrundikano wa mafuta kwenye seli za ini
Ugonjwa wa Fatty Liver (kwa kitaalamu Hepatic Steatosis) ni hali ambapo mafuta yanajikusanya kupita kiasi ndani ya seli za ini. Kwa kawaida, ini lina kiasi kidogo cha mafuta, lakini likiwa na zaidi ya 5–10% ya uzito wake ukiwa mafuta, hali hiyo inaitwa fatty liver.
Aina Kuu za Fatty Liver
1. Alcoholic Fatty Liver Disease (AFLD) – Hutokana na unywaji wa pombe kupita kiasi.
2. Non-Alcoholic Fatty Liver Disease (NAFLD) – Haisababishwi na pombe, mara nyingi huhusiana na:
Uzito kupita kiasi (obesity)
Kisukari aina ya 2
- Cholesterol na triglycerides nyingi
3. Non-Alcoholic Steatohepatitis (NASH) – Hii ni aina kali ya NAFLD, ambapo mafuta husababisha uvimbe na kuharibu seli za ini, inaweza kupelekea ugonjwa wa ini sugu au saratani ya ini.
Sababu Kuu za Fatty Liver
Uzito kupita kiasi au unene wa tumbo (central obesity)
Ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi
Kisukari aina ya 2 au insulini resistance
Mafuta mengi kwenye damu (cholesterol/triglycerides)
Kula vyakula vyenye mafuta mabaya na sukari nyingi
Kutokufanya mazoezi
Matumizi ya pombe (kwa AFLD)
Dawa fulani (kama steroids, methotrexate, tamoxifen)
Upungufu wa lishe (malnutrition) au kupungua uzito haraka
- Saratani au magonjwa mengine yanayoshusha kinga
Baadhi ya Dalili za fatty liver
Vidonda sugu vya tumbo, tumbo kuhisi kujaa gesi
Kupoteza hamu ya kula
Uchovu usioelezeka
Mkojo wenye rangi ya njano iliyo kolea au mkojo wa kahawiya
Miwasho sugu ya ngozi
Maumivu au usumbufu upande wa juu kulia wa tumbo
Homa ndogo na kichefuchefu (ikiwa kuna uvimbe)
Ngozi na macho kuwa ya njano (ikiwa imeendelea kuwa cirrhosis)
Madhara Ikiwa Haitatibiwa
Ini Kuendelea kuvimba siku hadi siku
Fibrosis (makovu kwenye ini)
Cirrhosis (ugonjwa wa ini sugu)
Saratani ya ini (hepatocellular carcinoma)
Kushindwa kwa ini (liver failure)
- Kifo kwa mgonjwa
Vipimo vya Kugundua
Vipimo vya damu: ALT, AST, GGT
Ultrasound ya ini
Fibroscan (kupima uimara wa ini)
CT scan / MRI
- Liver biopsy (kwa uthibitisho kamili)
Matibabu na Udhibiti
Matibabu ya ugonjwa wa mafuta ya ini huitaji dawa maalum isiyo na sumu wala kemikali hatarishi kwa afya ya ini na mfumo wa kinga
Tumia dawa zenye uwezo wa kuchoma mafuta mwilini na kurejesha seli za ini zilizo choka a kuchakaa pamoja na kuimarisha mfumo wa kinga
Punguza uzito taratibu (kupunguza 7–10% ya uzito wako kunaweza kupunguza mafuta kwenye ini)
Kula lishe bora yenye mboga, matunda, nafaka zisizokobolewa, protini konda
Epuka vyakula vyenye mafuta mabaya, sukari nyingi, na vyakula vilivyosindikwa
Fanya mazoezi angalau dakika 30–45 kwa siku, siku 5 kwa wiki
Epuka pombe kabisa
Kudhibiti kisukari, shinikizo la damu, na cholesterol
- Kuepuka dawa zinazoweza kuharibu ini bila ushauri wa daktari
Kwa huduma zaidi ya vipimo, chanjo na matibabu, unaweza kufika hapa kituoni kwakuweka appointiment kupitia website kwakujaza fomu inayo tokea mbele yako, kupiga simu au kutuna ujumbe mfupi wa maandishi kupitia WhatsApp +255628361104: