Search

Jisajiri - Weka appointiment


Jaza form hii kutengeneza account yako na kuweka appointiment yako.


Ngono ya mara kwa mara na homa ya ini


Baadhi ya madhara yanayoweza kumpata mgonjwa wa homa ya ini (hasa Hepatitis B au C) anaposhiriki ngono zembe ya mara kwa mara, hasa bila tahadhari:

𝗡𝗚𝗢𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗔 𝗡𝗔 𝗛𝗢𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗜


𝗞𝗮𝗺𝗮 𝗵𝗮𝘂𝗽𝗼 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗽𝗮𝗻𝗴𝗼 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗶𝗯𝗮𝗯𝘂 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗱𝗵𝗶𝗯𝗶𝘁𝗶 𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝘁𝗶𝗯𝘂 𝗯𝗮𝘀𝗶 𝗸𝘂𝗻𝗮 𝗵𝗮𝘁𝗮𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗲𝗻𝗲𝘇𝗮 𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝘄𝗲𝗻𝘇𝗮

Homa ya ini hasa aina ya Hepatitis B na C huambukizwa kwa njia ya damu na majimaji ya mwili (kama shahawa). Kushiriki ngono bila kinga huongeza hatari ya kumuambukiza mwenza.

 

𝗞𝘂𝗰𝗵𝗼𝗰𝗵𝗲𝗮 𝘂𝗵𝗮𝗿𝗶𝗯𝗶𝗳𝘂 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 𝘄𝗮 𝗶𝗻𝗶

Ngono ya mara kwa mara inaweza kuongeza msongo wa mwili, na kwa wagonjwa wa ini, inaweza kuchochea uharibifu zaidi wa seli za ini.

 

𝗛𝘂𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗶𝗮 𝗵𝗮𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗻𝗴𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝘄𝗶𝗹𝗶 𝗸𝘂𝘀𝗵𝘂𝗸𝗮 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶

Mwili wa mgonjwa wa homa ya ini huwa na kinga iliyoathirika. Ngono ya mara kwa mara bila kupumzika yaweza kuchosha mwili na kuathiri zaidi uwezo wa kupambana na virusi.

 

𝗞𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝗵𝗮𝘁𝗮𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝗺𝗮𝗽𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮 𝗺𝗲𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝘆𝗮 𝘇𝗶𝗻𝗮𝗮

Mwili wa mgonjwa wa homa ya ini huwa dhaifu zaidi, hivyo ni rahisi kuambukizwa magonjwa mengine kama UKIMWI, kaswende, na kisonono.

 



𝗞𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝘂𝗰𝗵𝗼𝘃𝘂 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗿𝗮

Mgonjwa wa homa ya ini mara nyingi hupata uchovu. Ngono ya mara kwa mara bila kupumzika inaweza kuongeza uchovu na kuchangia kudhoofika kwa afya.

 

𝗞𝘂𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗮 𝗺𝗽𝗮𝗻𝗴𝗼 𝘄𝗮 𝘁𝗶𝗯𝗮

Tiba za homa ya ini huhitaji nidhamu na mapumziko. Shughuli nyingi za kimwili kama ngono zisizo na mipaka huweza kuathiri ratiba ya dawa au kupunguza ufanisi wake.

 

𝗠𝗮𝘂𝗺𝗶𝘃𝘂 𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗺𝗯𝗼 𝗮𝘂 𝗶𝗻𝗶 𝗸𝘂𝘂𝗺𝗮 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶

Ngono yenye nguvu au mara kwa mara inaweza kuchochea maumivu upande wa ini, hasa kwa wagonjwa walio kwenye hatua ya kati au mwisho ya ugonjwa.


𝗛𝗮𝘁𝗮𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝘂𝗷𝗮𝘂𝘇𝗶𝘁𝗼 𝘆𝗮𝗻𝗶 𝗺𝗶𝗺𝗯𝗮 (𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗮𝘄𝗮𝗸𝗲 𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗺𝗮𝗮𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶)

Mwanamke mwenye homa ya ini anapopata mimba anaweza kumuambukiza mtoto kupitia mzunguko wa damu au wakati wa kujifungua, hasa kama hajapatiwa chanjo au matibabu.

 

𝗞𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝗺𝘀𝗼𝗻𝗴𝗼 𝘄𝗮 𝗸𝗶𝘀𝗮𝗶𝗸𝗼𝗹𝗼𝗷𝗶𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗺𝗴𝗼𝗻𝗷𝘄𝗮

Hali ya kuogopa kumuambukiza mwenza au kuishi na hatia baada ya tendo inaweza kuathiri afya ya akili na kusababisha msongo wa mawazo au huzuni.

 


 

𝗧𝗔𝗛𝗔𝗗𝗛𝗔𝗥𝗜..:

Ni muhimu kwa wagonjwa wa homa ya ini kutumia kinga (kondomu), kuzungumza na daktari kuhusu hali yao ya kiafya, na kuwa wazi kwa wenza wao kuhusu hali ya maambukizi. Pia kujizuia kushiriki ngono wakati wa matibabu makali au wakati wa kushuka kwa kinga ya mwili ni jambo la busara.


𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔:-  Ni muhimu kufuatilia afya yako kwa kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuyafikia matibabu ya mapema pale tatizo linapo bainika, kwani kila sekunde ni muhimu katika kuokoa maisha na kuepuka madhara ya kudumu.


𝗞𝗮𝗿𝗶𝗯𝘂 𝘁𝘂𝗸𝘂𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗶𝗲 𝗸𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘇𝗮 𝗮𝗳𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗻𝗮𝘁𝗼𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗩𝗜𝗣𝗜𝗠𝗢, 𝗨𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔𝗕𝗨.

Taarifa zaidi

Karibu kwa huduma!